Sunday

UKIMYA WA MATONYA KUMBE YUKO SHULE ANASOMA KENYA.


Watu walikuwa wakijiuliza Matonya yuko wapi mbona kimya, hatimaye nimefumana nae maeneo fulani na kuniambia kuwa alikuwa kwenye tour huko Mombasa Kenya. Ila wakati yupi Nairobi alikuwa studio akitengeneza wimbo na msanii wa huko huko Nairobi anajulikana kwa jina la Nonini, mbali na Nairobi pia ameshatengeneza biti kwa producer Dunga na akirudi anaishughulikia na wimbo huo ameupa jina la "UTAKWENDA KULA ULIPOPELEKA MBOGA"

Pia Matonya amenidokeza kwa sasa anapiga kitabu kule Kenya ila amesema ni mapema sana kusema anachokisomea mpaka akipata cheti ndio atasema alikuwa anasomea nini. Kwahiyo amewaomba mashabiki wake kwa sasa wawe wapole tu mnyamwezi wenu atakuwa kitaani muda si mrefu.

No comments: