Friday

NARUDI DENMARK KUISHI NA FAMILIA YANGU "JCB"


Mtu mzima JCB hivi sasa yuko njiani anaelekea Nairobi tayari kwa safari yake ya kwenda Denmark kuishi na familia yake. JCB ameongea na DJCHOKAblog kwa njia ya simu akitokea Arusha akielekea Nairobi kwaajili ya kupanda ndege itakayompeleka hadi Amsterdam halafu Denmark. Alipoulizwa kuhusu atarudi lini JCB alijibu bado hajafikiria labda mwakani ndio atarudi ila atakaa kaa sana huko Denmark na mke wake pamoja na mtoto wao mmoja waliompata

Taarifa kuhusu mabadiliko ya ngazi za ufaulu Tanzania, hakuna tena division 0

wanafunziSerikali ya Tanzania imetangaza kufuta daraja sifuri katika matokeo ya elimu ya sekondari nchini na kuongeza daraja la tano ambapo pia matokeo ya kidato cha nne kwa watahiniwa wanaorudia mitihani yatahusisha matokeo yao ya awali wakati wakiwa shuleni ili kuwarahisishia kupata alama nzuri.
Katibu mkuu wa Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome amesema pamoja na marekebisho hayo pia wameongeza daraja B ya juu kwa alama za ufaulu ambapo daraja A wigo wa ufaulu ni kati ya alama 75 na 100, daraja B la juu ni kati ya alama 60 na 74, daraja B la kati ni 50 na 59, daraja C kati ya 40 na 49, daraja D kati ya 30 na 39, daraja E kati ya 20 na 29 na daraja F ni kati ya alama 0 na 19.
Profesa Mchome amesema marekebisho hayo yanalenga kuinua kiwango na kuboresha kiwango cha elimu Tanzania ambapo kwa kila muhitimu wa kidato cha nne matokeo yake ya mwisho yatajumlishwa na alama zisizozidi 40 ambazo zitatokana na majibu ya mitihani ya kidato cha pili, cha tatu na mtihani wa Mock.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba mtihani wa kidato cha nne utafanyika November 4 2013 ambapo zaidi ya Watahiniwa laki nne wanatarajiwa kufanya mtihani hii ambapo kati yao, Watahiniwa laki 3 na elfu 67,399 ni kutoka shuleni huku Wavulana ni 198,257 sawa na asilimia 53.69 na Wasichana ni 169,142 sawa na asilimia 46.04 ambapo vituo vya kufanyia mitihani ni 4,365