Wednesday

MKALI WA RnB TOKA TANZANIA....Q JAY AOKOKA!


JOSEPH KELVIN MAPUNDA AKA Q-JAY
Mkali wa RnB Tanzania ambaye kwa sasa anaendelea kula matunda ya ndoa,Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay kwa sasa ameokoka na kuamua kumfuata yesu!
Q-Jay amekuwa akitolea nje concert kibao ambazo anaalikwa kwa ajili ya kufanya show,kutokana na imani yake mpya aliyonayo sasa,na amefunguka kuwa “mziki niliokua nafanya ulikua ni wa dunia na ningewashauri wasanii wenzangu wote wanaoimba nyimbo za dunia kuufata wokovu na kuachana nazo,kwa sasa nimepumzika kufanya shughuli za mziki lakini kuanzia mwezi wa sita nitaanza kurekodi mziki yangu mipya ya kumtukuza mungu yaani gospel na natarajia kutoa album”....alimalizia Q Jay kwa sauti pole ya kilokole,akifuata nyayo za Stara Thomas,K Basil na Renee Lamira!
....ENZI ZA WAKALI KWANZA...Q-JAY NA MAKAMUA WAKIFANYA MIZIKI YA KIDUNIA!
Q-Jay alianza 'muziki wa kidunia' akiwa na kundi la RnB,Wakali Kwanza na kina Joslin,Makamua na wengine kibao na mara ya mwisho walitoa album ya pamoja na Makamua wakiwa chini ya MJ Records na nyimbo zake za kidunia kama Sifai featuring Joslin,na collabo kama Kitu Gani,Nakupa Sifa alizinukisha vilivyo

No comments: