Thursday

DIDDY AWASHUKIA RAPPERS WANAOMTUHUMU KWA UTAPELI


Hivi karibuni mtu mzima Puff amekanusha uvumi uliokua umeenea kwa siku nyingi kuwa aliwapunja mkwanja na kuwamistreat wasanii waliopitia katika Label yake ya BAD BOYS, kwa miaka mingi radio mbao zilikua zikeneza taarifa kuwa BAD BOY'S CEO anawadhulum wasanii wake na taarifa hizi zilikua zikipata nguvu hasa inapotokea wasanii kuhama label hiyo, wengi wao hawakuondoka kimya kimya kwani kulikua na kurushiana maneno ya hapa na pale kati yao na Diddy, kati yao ni The Lox, Mase na wengineo.

Kuweka sawa uvumi huo, Diddy ametumia kurasa za VIBE MAGAZINE ya mwezi huu na ndani yake amefunguka ya moyoni.

Diddy amesema hajawahi kufanya kitendo chochote kibaya kwa Wasanii wote aliowatoa, akaongeza kuwa yeye asibebeshwe lawama kwa wasanii ambao hawakuwa na mafanikio ya muda mrefu, jamaa anasema"itakua unanijengea picha mabayo siyo, kwa mtu kama mimi niliyekuzwa kwa misingi ya kufanya kazi kwa kujituma na kula jasho langu, na si kutumia au kunyonya jasho la mtu mwingine, siku zote najaribu kusaidia watu lakini watu hawaifahamu Game vizuri, kwani msanii anakua na uhai mfupi sana kimuziki



Diddy anaendelea kusema kuwa: haiwezekani mimi kuwa Jay- Z, LL ama Nas, yaani hiyo haitowezekana, hao hawafikii hata asilimia moja ya marapper wote, kama utamwangalia msanii yeyote aliyekua Ruff Ryders, wako wapi? kama utachek wasanii waliokuwepo Def Jam kipindi kile Tunaanza wako wapi? waliokuwepo Roca-A-Fella, Jive wako wapi? si kwamba kuna kitu walikosea, cha msingi Msanii anakua na miaka minne mpaka mitano ya Kuwepo kwenye Game, hicho ndo kitu nilichotaka kusema siku nyingi.

No comments: