Friday

Young Buck kumpeleka 50 Cent mahakamani

Baada ya kuzuiliwa kwa mali zake na TRA ya Marekani IRS, Memba wa zamani wa kundi la G-Unit inaripotiwa kuwa ameamua kutafuta msaada wa Kisheria kutokana na mgogoro wa kimkataba kati yake na 50 Cents, ambae inasemekana bado ana shikilia umiliki wa mkataba kati ya Young Buck na G-unit.

Kwa mujibu wa Nashville City Paper, Young Buck ana mpango wa kudai dola milioni tano, kutokana na na kubaniwa Kumshirikisha na msanii yeyote kwenye ngoma zake, lakini pia mtu mzima kwa kipindi chote alichotemwa na Kundi hilo miaka mitatu iliyopita, Label hiyo haija release ngoma yake yoyote, pamoja na 50 Cents wengine wanaoshtakiwa ni SHA MONEY XL na G-Unit.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa Young Buck, kesi hiyo itafunguliwa ndani ya siku 30-60

Kama unakumbuka Young Buck aliwahi kulalamika kuwa 50 Cents anataka yeye afilisike, kwasababu baada ya kumtema kwenye kundi la G-Unit aliendelea kumshikilia kimkataba kwenye label ya G-unit kwa hivyo Young Buck hakuweza kurelease ngoma yoyote ya Kibiashara/Commercial Song nje ya label hiyo, lakini pia kila alipokwenda studio jamaa waliziponda idea zake na alipotaka kuwashirikisha wasanii wengine katika ngoma, 50 alicrush vibaya mno.

Mpaka hivi karibuni IRS walipomtimbia nyumbani kwake na vitu vyake kibao vyenye thamani. http://api.ning.com/files/fW2QiYuodgtrhcXatd81fnTl0-0GOrZhODi9NYD-4itOYr5Pb8VLix*gCXkqgqHr3GS0dPUMuAmuf19lIncOcgYtDiidprWX/young_buck_4.jpg

No comments: