Saturday

ROGERS APATA SHAVU UFUNGUZI TAMASHA LA BUSARA

Mkali wa Gitaa Baridi, Mwanamuziki Rogers Lucas ataupamba ufunguzi wa Tamasha la 13 la nchi za Jahazi. Imethibitishwa.
Rogers Lucas, Mshindi wa pili wa Bongo Star Search mwaka 2008 atafungua pazia la burudani za Tamasha hilo lilipangwa kuanza leo katika uwanja wa Ngome Kongwe, mji Mkongwe Zanzibar.
Tamasha hilo ambalo linatazamiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 2000 kutoka kila kona ya Dunia limepangwa kukoma tarehe 18 July Mwaka huu ambapo zaidi ya filamu 100 zitakuwa zimeonyeshwa na vikundi zaidi ya 20 zitakuwa vimetumbuiza.
Rogers ambaye amepangwa kufungua tamasha hilo atafuatiwa na wanamuziki wengine kutoka Bagamoyo Kjetil Haugbro na kikundi cha kusheki cha D 6 cha Zanzibar pamoja na Mshiri Mahiri Zanzibar Amina.
Rogers anazungumzia mualiko huwa kuwa ni heshma ya kipekee huku akieleza nia yake ya kufanya makamuzi ya kufa mtu.
Msanii huyo anayeendelea kutamba na kibao chake ‘Rudi’ amepanga kuvurumisha vibao vyake kadhaa kutoka katika Albam yake mpya yenye jina la Rudi inayotamba na vibao nane ambavyo ni Jasho la Upendo, Ni wewe, Mama, Niambie Leo, Si Utani, Hayupo na Rudi wimbo uliobeba jina la Albam hiyo.
Albam hiyo ni moja ya Albam bora zilizowahi kutolewa na wanamuziki huyo katika muziki wa BongoFleva hapa nchini. Albam ya Rogers iko tayari madukani na inapatikana katika CD vile vile.
Rogers kijana mtulivu anayelimudu vyema gitaa lake amekuwa akipata mialiko kadhaa katika nchi za Magharibi kama Ujerumani Uswisi na Australia .
Mbali na umahiri wake katika muziki wa aina yake Rogers pia amewahi kushirikiana na mwanamuziki mwenzake mkubwa ajulikanaye kama Ricardo Flecha kutoka Paraguay Amerika ya kusini mwanamuziki ambaye anaheshimika sana katika ukanda huo kwa uwezo wake katika kupiga muziki.
Kwa kopi ya albam yake wasiliana naye kupitia No.
0716954854
Au Email:
Rogerstht@yahoo.com
www.rogerslucas.com

No comments: