Saturday


Mimi ni mwanaume wa miaka 32, nimeoana na mke wangu sasa ni mwaka wa 4 na tuna mtoto mmoja. Nilikutana na huyu rafiki wa mke wangu miaka mitatu iliyopita tulipoamia Dar kikazi toka Mwanza nilipokuwa nafanyia kazi kabla. Nilipomwona tu nilimtamani na yeye hakuwa na hiyana, tukaanza mahusiano ya mapenzi kwa siri. Mahusiano yalipamba moto na siwezi kuhesabu ni mara ngapi nimefanya naye mapenzi. Kuna wakati nilitaka kuachana nae lakini alinitishia kuwa nikifanya hivyo ataharibu ndoa yangu, na ntakuwa nimekosa kila kitu. Nikiwa nae na mke wangu pamoja ninachoweza kufanya ni kutabasamu tu na siongei nae sana. Mke wangu anajuaga kuwa namchukia rafiki yake mana anaona huwa simchangamkii kivile kama wengine. Maskini, kumbe ni kinyume chake. Sasa nimechanganyikiwa mana ananiambia ana mimba yangu. Kwakweli sijui nifanyeje, mana nikifikiria tulipotoka na mke wangu na jinsi ninavyomsaliti kwa rafiki yake, roho inaniuma, ila ndo hivyo na naiweka ndoa yangu pabaya na nikifikiria na mtoto tena. Naomba wadau wa Mapenzi bongo wanipe ushauri.

No comments: