Saturday


Jamani naombeni msaada wenu nimeoa yapata mwaka wa 4 na tumejaliwa mtoto mmoja wa kike; Baada ya miaka miwili,Ndoa yetu imekumbwa na misukosuko mingi sana ikiwa ni pamoja na mwenzangu kupunguza kunipa haki yangu ya ndoa hadi kufikia miezi 3 (hapo kabla tulikuwa tukipumzika wakati akiwa kwenye period tu na mara nyingi sana yeye ndiye alikuwa akinichokoza; alianza na kunipunguzia ikawa mara moja kwa wiki; mara hataki tushiriki mchana ama asubuhi anataka usiku tuu na akiwahi kulalal hawezi kuamka tena na hata kwenda kuoga na mimi ndio kabisaaaa )na siku ya kupewa inakuwa kama anatimiza wajibu na ni round moja tu. Hali hii ilinishinda na kwa kweli niliamua kutoka nje ya ndoa yangu hii ikiwa ni baada ya kumsihi na kumtafadhalisha sana mke wangu juu ya jinsi nilivyokuwa najisikia nakereka ; jibu lake likawa yeye haoni tatizo na sio lazima tufanye mapenzi ndio nijue ananipenda!Hatimaye mke wangu akajua; sikumficha nilimweleza sababu na nikamwomba msamaha ikiwa ni pamoja na kumsihi kujali hisia zangu; hali ilitulia kidogo lakini masharti yakaongezeka aligoma nisimwendee chumvini na yeye akawa hataki kuniendea ilhali ni mchezo amabo mimi na yeye tumejifunza pamoja na tuliupenda sana hapo kabla; nilivumilia lakini miezi miwili baadae hali ikarudia kama ya zamani; nikitaka game nakuwa nafanya booking na mbaya zaidi style ikawa ni moja tu; kifo cha mende eti yeye ndo inamfurahisha zaidi lakini kibaya ikafikia nikitaka game lazima nimseme wee na siku nyingine nanyimwa tu bila hata maelezo; nikaamua kumfanyia upelelezi na kungamua kuwa alikuwa ana mahusiano yasiyo rasmi nje ya ndoa! nilikusanya ushahidi na kumface ambapo alikiri kufanya hivyo ikiwwa ni revenge kwangu eti haamini kuwa nimeachana na wanawake wa nje ; aliniomba msamaha nami kwa kukumbuka kuwa yeye ni mama mtoto wangu na alinisamehe huko nyuma ; nikamsamehe na tukaendelea kuishi; roho ilimiuma kwa kujutia niliyoyasabisha lakini niliamua kumsamehe ili kupona mimi binafsi. Tatizo limekuja sasa tumerudia hali hiyo tangu mwaka huu uanze nimepewa penzi mara moja; visingizio kila uchao mara kichwa kinauma mara tumbo limejaa gesi, mara period imekuwa ndefu mno hivyo napumzika ilimradi nashindwa kuelewa ikiwa bado ana mapenzi na mimi ama la ? Kwa kweli mimi nampenda sana na hasa has nikiona anavyomlea mwanetu na hata kunijali mimi kwa malazi na chakula; lakini namhitaji yeye kama mke wangu anchanganyikiwa nifanye nini!Kutoka nje tena sitaki kwani sikuona faida ya penzi la kuiba.Baba Rachel

No comments: