Monday

50 Cents amdiss Mitchell Obama


Watu kibao wamecomment juu Twiter alizokua akituma 50 Cents jana, katika Twiter hizo Fif amemdiss First lady wa Marekani Mitchell Obama, Nicole Bitchie, Rick Ross na watu wengine. Kuna mtu ameandika kuwa Fif anataka Attention kutoka kwa watu na vyombo vya habari, kuna wanaoamini kuwa mchizi amedata, lakini wengine hawaamini kuwa ni 50 aliyendika Tweet hizo yaani huenda kuna mtu amehack account yake ya Twitter so anaitumia vibaya ili kumchafua 50 Cents aonekane hana maana kwa Funs

Katika moja ya Tweet, 50 Cents ameandika “ look Mitchelle Obama need one thug in her life …..ck that come here Girl you can be my Mentor”

Thursday

DIDDY AWASHUKIA RAPPERS WANAOMTUHUMU KWA UTAPELI


Hivi karibuni mtu mzima Puff amekanusha uvumi uliokua umeenea kwa siku nyingi kuwa aliwapunja mkwanja na kuwamistreat wasanii waliopitia katika Label yake ya BAD BOYS, kwa miaka mingi radio mbao zilikua zikeneza taarifa kuwa BAD BOY'S CEO anawadhulum wasanii wake na taarifa hizi zilikua zikipata nguvu hasa inapotokea wasanii kuhama label hiyo, wengi wao hawakuondoka kimya kimya kwani kulikua na kurushiana maneno ya hapa na pale kati yao na Diddy, kati yao ni The Lox, Mase na wengineo.

Kuweka sawa uvumi huo, Diddy ametumia kurasa za VIBE MAGAZINE ya mwezi huu na ndani yake amefunguka ya moyoni.

Diddy amesema hajawahi kufanya kitendo chochote kibaya kwa Wasanii wote aliowatoa, akaongeza kuwa yeye asibebeshwe lawama kwa wasanii ambao hawakuwa na mafanikio ya muda mrefu, jamaa anasema"itakua unanijengea picha mabayo siyo, kwa mtu kama mimi niliyekuzwa kwa misingi ya kufanya kazi kwa kujituma na kula jasho langu, na si kutumia au kunyonya jasho la mtu mwingine, siku zote najaribu kusaidia watu lakini watu hawaifahamu Game vizuri, kwani msanii anakua na uhai mfupi sana kimuziki



Diddy anaendelea kusema kuwa: haiwezekani mimi kuwa Jay- Z, LL ama Nas, yaani hiyo haitowezekana, hao hawafikii hata asilimia moja ya marapper wote, kama utamwangalia msanii yeyote aliyekua Ruff Ryders, wako wapi? kama utachek wasanii waliokuwepo Def Jam kipindi kile Tunaanza wako wapi? waliokuwepo Roca-A-Fella, Jive wako wapi? si kwamba kuna kitu walikosea, cha msingi Msanii anakua na miaka minne mpaka mitano ya Kuwepo kwenye Game, hicho ndo kitu nilichotaka kusema siku nyingi.

Kanye West Kuachia Ngoma mpya kila Ijumaa


Mtu mzima Kanye West inaonekana ana mizuka ya Christmas wiki 18 kabla ya muda kufika, nasema hivyo kwa sababu hivi karibuni kupitia mtandao wa Twitter ametangaza kuwa atakua anachia ngoma mpya kila siku ya ijumaa mpaka msimu wa X-mas ufike, mchizi ame Tweet mara tatu na inabidi nikusomee zote kama alivyoandika:

" najua wote mnapenda ngoma mpya, so nitakua naachia ngoma moja mpya kila weekend mpaka X-Mas, itakua ngoma yangu ama ya Jay. Tweet ya pili na Tatu ameandika: "naita ni good Friday, wote jueni kwamba kila ijumaa nitakua naachia new Joint kutoka kwenye familia yetu, tunaicheki Game tofauti kabisa.

Its about the Funs,haina kurudi nyuma, Thats why i dropped see me now, it wasn'nt about me it was about the Summer the BBQs e.t.c

Mtu mzima Kanye mwishoni mwa mwaka huu pia natarajia kudondosha Album……mwanzo aliita Good ass Job lakini baadae akaonesha wasiwasi na jina hilo so akasema kuwa bado anafikiria jina la album hiyo.

LIL WAYNE AKIWA SELO.

KAMA UNAMTAFUTA FID Q YUPO NA FAT JOE

Saturday

VITU VYA KUTUSAIDIA KUONGEZA FURAHA KATIKA MAISHA YETU




1.Kujitambua na kujipenda wewe mwenyewe
2.Kuwa rafiki mzuri kwa mwenzi wako mume/mke,watoto,wafanyakazi wenzako,wazazi wako,ndugu zako,wateja wako n.k

3.Kama unafanya kazi ipende kazi yako.
4.Jivunie ulichonacho katika maisha kwa sasa na usiwe mtu wa kulalamika.Hesabu baraka zako pia.
5.Tujifunze kusamehe, tuishi bila vinyongo6.Jifurahishe mwenyewe…kwa kusikiliza muziki kama unapenda muziki ,movies,michezo mbalimbali kama mpenzi wa michezo,mazoezi n.k
7.Ijali afya yako kwa kufanya vipimo pindi unapojisikia afya yako haiko sawa,usiipuuze ili uendelee kuwa na afya njema na mwenye furaha pia.Ukiwa na afya njema utaweza kufanya hayo yaliyoorodheshwa mwanzo vyema.
8.Dini….ishike dini yako inasaidia kukupeleka katika njia iliyo sawa.

Ni baadhi ya mambo niliyojifunza nikaona sio mbaya kuweka hapa kwenye ubao wetu maana kila siku tunajifunza.

WYCLEF JEAN HONGERA

Tuesday

EBWANAA HII NOMA


Robert kelly

EBWANAA HII NOMA


SEMA CHOCHOTE JOMBAA

UNAPOMKUTA RAFIKI YAKO KIPENZI CHUMBANI KWAKO AKIWA NA MPENZI WAKO UTAFANYAJE?

Hebu tujadiliane hili; Unaishi jijini Dar es Salaam, unaye mpenzi wako ambaye unampenda sana. Huyo alikuwa akiishi mkoani Mbeya, lakini amekuja Dar kama wewe kutafuta maisha. Mkakutana na kupendana, baadaye mkaamua kuanza kuishi pamoja.
Lakini unaye rafiki yako kipenzi, ambaye unamuamini na kumuheshimu sana. Mara nyingi amekuwa akija kukutembelea nyumbani jioni na mnashiriki pamoja chakula cha usiku mara nyingi. Siku moja ukiwa ofisini, unagundua kwamba kuna kitu ulikishau nyumbani, unaamua kurudi kwa ghafla.
Ile unaingia sebuleni, unashangaa kukuta nguo za mwanaume pamoja na viatu, ulipoenda chumbani, unamkuta mpenzi wako yupo utupu na rafiki yako, wakiwa katika maandalizi ya kufanya mapenzi.
Pambanua ubongo wako. Kama ni wewe utachukua hatua gani? Tujadiliane.href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEvIyewWAPj7_OnDSHfwtjHjAbFi9PSEg6-h794f714mHRtu8h9PSm0HfJWRJ1tVz1g8QvjvyiQGAqviKHQ6QARck0tZi9GbKX_lNVCgOg1coUHH0fy-VYTOQCiITLQyx0gsE3b4-eyd4/s1600/mahabaa.jpg">

JOMBAA BOGA HILO


Hivi unaweza kusema nini kuhusiana na uhusiano wa
jinsia moja.

MPENZI WAKO ANAPOACHA KUJIBU SMS ZAKO, ANAMAANISHA NINI?



Hi, marafiki! Muda kidogo nilikuwa sipo, mambo yanabana sana, lakini leo nimeamua kurudi. Naanza na hili, mpenzi wako anapoacha kujibu meseji zako unamchukuliaje?
Iko hivi, wapenzi wengi wanapenda sana kupewa nafasi ya kwanza kwa kila kitu, hakuna ubishi wapo sahihi na wana haki ya msingi kabisa!
Hebu vuta picha, fikiria kwa makini, unaye mpenzi wako, ni mchana upo kazini, upo busy sana, lakini ukakumbuka kuwasiliana naye japo kwa sms ya kichokozi tu; "Hi sweet, are u ok? Umekula nini leo? Luv u..." ukaituma kwa mwenzi wako.
Tena sikia, baada ya mpenzi kutuma sms ya love kama hiyo ambayo hasa inakuwa inamu-wish mlo mwema, anakuwa anasubiri majibu yake kwa hamu kubwa sana, lakini giiiii....hakuna majibu wala ma-answer.
Unadhani nini kinasababisha hili kutokea? Na kama ungekuwa wewe umetuma sms kama hii kwa mwenzi wako, halafu hajajibu, unachukuliaje?
Weka maoni yako, halafu nitakuja na tip zangu, nitakuwambia nini husababisha na nini cha kufanya ili kuweza kumjua mwenzi wa aina hii.
Karibuni tuchangie...

WATOTO WAZURI


jamani kizuri kipeni
huyu mtoto mzuri sana

MAPENZI MABAYA


Jamani mapenzi noma kweli
check huyu mzee anavyowaza

JAMANI WANAPENDA HAWA


KAMA NA NYIE MNAPENDANA SEMEN

Thursday


Maisha jinsi yalivyo sasa hivi hatuhisi kwamba mtoto wa kiume anatakiwa kuandaliwa kuishi na mtoto wa kike wa kisasa?.Zamani mtoto wa kike alikuwa alikuwa anaandaliwa mapema nyumbani namna ya kuwa mke wa mtu na majukumu ya kifamilia.Lakini kwa sasa mtoto wa kike anahimizwa kuhusu suala la shule kwanza,kazi nzuri,na mwisho kabisa ndio kuwa mke mtarajiwa.

Msichana huyu anapokuja kukutana na mtoto wa kiume kuanzisha familia wote watakuwa na sauti,mwanaume akiongea ujinga mwanamke atamkosoa kwamba hapana hapo sio hivyo ni hivi.Na pia kwa muda kumekuwepo na ile hali ya wanaume kuogopa wanawake wasomi kwa sababu wanasema wanajifanya wajuaji.Ila kwa sasa imefika wakati mwanaume pia atambue kuwa kuwa na mwanamke msomi sio kukaliwa kichwani hapo ndipo tunahitaji kumuandaa namna ya kuishi na mtoto wa kike wa kisasa...shule kwanza,kazi,halafu ndio kuishi na mume.

INAPOTOKEA UMEALIKWA CHAKULA NYUMBANI KWA NDUGU,RAFIKI AU JAMAA ZINGATIA YAFUATAYO.


1.Usitoe comment mbaya kuhusu chakula unachokula maana kuna mtu amejiandaa sana kupika hicho chakula .
2.Usiongee ukiwa na chakula mdomoni
3.Onyesha kufurahia chakula
4.Kama unahitaji kitu kama chumvi,bakuli ya mboga au chochote na haufikii omba usogezewe na sikupitisha mikono kwa mwenzako ambae tayari anakula.
5.Usitoe kitu mdomoni ukakiweka juu ya meza,kama ni mfupa toa mdomoni weka pembeni kwenye sahani yako.
6.Usibeue/kutoa gas kwa sauti...
7.Ukialikwa mlo kwa rafiki,ndugu au jamaa baada ya mlo shukuru na ueleze ni namna gani umefurahia chakula ulichokula unaweza ukasifu mboga kwa mfano labda "samaki alikuwa mtamu kapikwaje maana kama sijawahi kula samaki.."

na mengineyo tunaweza kukumbushana.

Wednesday

ALIYEJIFANYA MENEJA WA DRAKE KIZIMBANI


Jamaa mmoja kutoka Milwaukee, Wisconsin nchini marekani, anashtakiwa kwa kujipatia pesa kinyume cha sheria, na hiyo ni baada ya kujifanya yeye ni manager wa Lil Wayne na Drake. Kwa mujibu Document za shtaka lililofunguliwa na kampuni Eagles Intertainment Inc, inasemekana mshtakiwa Joey Turner Jr. a.k.a Jo Flowrushus, alijifanya yeye ni Cortez Bryant ambae ni meneja wa Drake so ana mamlaka ya kusimamia booking zote za Drake.

Joey Turner aliwasiliana na Eagle Intertainment kwamba Drake anataka Dola elfu 90 kwa ajili ya show, na kampuni hiyo ilitoa Dola elfu tisa kama Deposit ya show hiyo ambayo ilitakiwa kufanyika tarehe moja Septemba, katika miji wa Milwaukee Wisconsin. Kesi ipo mahakamani, na Kampuni ya Eagle Intertainment inataka ipewe

Na mtuhumiwa dola elfu 27, kufidia gharama za kumlipa mwanasheria na gharama ya kufungua kesi hiyo mahakamani. Kampuni inayohusika na bookings za Drake ni International Creative Management pekee.

NATURE, KIBA, ALADJI NA NGWEA WAFUNIKA CLOUDS TV, MTV BASE PARTY



mzee wa alge
nature akifanya makamuz
ngwear

Saturday


Like a finely-crafted automobile, Nelly is taking the necessary steps to ensure his new album is ready for the road. He’s a**embled today’s hottest producers, a fleet of high-profile collaborators, and polishing it all off with a fall release date.Universal Motown will unveil the St. Louis rapper’s sixth studio album 5.0 on November 16. The club jam “Tippin’ in da Club,” produced by Dutch, sets the tone for the high-octane record. The song has already gone to urban radio, while the second single “Just a Dream” has been serviced to Top 40 stations. The latter was produced by Jim Jonsin and Rico Love.
“It’s a lot of things,” Nelly told Rap-Up.com about the album title’s significance. “It’s also my fifth drop date. It’s just the energy of it all. [The Mustang] 5.0 was always one of my dream cars. As soon as I had enough money to buy one of these mothaf***ers, they stopped making these s****.”

The follow-up to 2008’s Bra** Knuckles is set to feature production from Dr. Luke, Polow Da Don, Don Vito, and Smash Factory, and guest spots from T.I., Akon, Diddy, and Kelly Rowland on “Gone,” the sequel to their 2006 smash “Dilemma.”

But he’s not trying to repeat history with his latest collaboration. “Let’s be honest, we can’t do ‘Dilemma’ over again. That’s etched in time,” he said. “It is what it is; that song was for that point in time.”

Sunday

Album Cover ya Fabolous yatoka kwenye mtandao



Album Cover ya mtu mzima Fabolous, imetoka kwenye mtandao, na ina tarajiwa kutoka mapema mwezi wanane tarehe 31, itaitwa There Is No Competition 2: The Grieving Music Mixtape. katika Cover ya album hiyo mtu mzima Fabulous ametupia nguo nyeusi miwani myeusi yaani full black kasoro saa na bracelate aliyovaa ndo vina rangi ya Gold, jamaa ameshow respect kwa wafu kwani nyuma yake linaonekana jeneza likiwa limefunguliwa na tukio hilo lote background yake ni jumba lililojengwa kwa style ya kiroman, and adefinatly this must be a church, ndani ya Mix Tape hii mpya mtu mzima Fabulous amechukua ngoma sita kutoka kwenye mixtape iliyopita inaitwa Funeral Service Mixtape na ngoma 2 ni mpya zinaitwa “Lights Out” and “Girl You Be Killin’ xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kanye West anakuna kichwa kupata jina album baada ya kulikacha jina la Good ass Job Kanye west halitaki jina la Good ass Job kuwa jina la album yake anayotarajia kuitoa mwezi wa tisa mwaka huu, jamaa anasema anakuna kichwa ili aweze kupata jina jipya Jana Kanye West alifungua Twiter page mpya, na alitumia muda wake kujibu maswali ya Funs wake, ambapo walimuuliza ataipa jina gani album yake? jamaa akajibu Good ass Job si jina la album yangu, nina kuchagua kati ya majina mawili niliyopata, rapa hyo hakuweza kutaja ni majina gani hayo..
Kama unakumbuka mchizi aliwahi kusema kuwa ataendelea kutumia theme za kicollege kama kawaida ya majina ya album zake, kama The College Dropout, Late Registration, and Graduation, na Good ass Job ilikua iwe ya mwisho kwenye series/ mpangilo huo.

Jamaa angenipa chance ya kumchagulia jina la album hii ningemwambia kabla ya Good ass Job atumie jina la Job less hivi au design yoyote ya jina la kumaanisha yaani baada ya Graduation ni kijiweni kibongo bongo
Album ya tano ya mtu mzima Kanye inatarajiwa kutoka September 14

Nicki Minaj akanusha album yake Kuleak


Young Money member Nicky Minaj amewahakikishia Rap Fans kuwa ngoma iliyoleak kwenye Internet kuwa haipo kwenye album yake anayotarajia kuiachia mwishoni mwa mwaka huu. Akiwaandikia followers wake wanaokadiriwa kufikia milioni moja katika mtandao wa Twitter, jana mchana Nicki Minaj alikanusha ku leak kwa album hiyo. Amesema ngoma iliyo leak ni ya zamani. Pia mwanadada huyo akasema Video ya ngoma yake itakuwa kwenye iTunes hivi karibuni. Kama unakumbuka Mshkaji wake wa karibu Drake aliwahi kupatwa na balaa la kuleak kwa album yake ya Thank me Later, na kitu kama hicho huweza kusababisha mauzo ya album husika kutokufanya vizuri wakati itakapotoka. Nicky anatarajia kutoa album yake Novemba 23 mwaka huu, bado hajaipa jina na wakati watu wanasubiri atoe jina basi waiite Nicki Minaj: The album.

Jennifer Lopez apata deal ya kuwa judge ‘American Idol’


Waswahili wanasema mwenye nacho huongezewa, Ana igiza, ana imba, ana dance vizuri mno, vile vile ni mjasiriamali, mpaka hapo unajua namzungumzia Nani? Namzungumzia mwanadada Jennifer Lopez uanweza muita J-Lo, pamoja na kuweza kumudu mambo hayo yote niliyoyataja, hivi karibuni amesign deal ingine kali ya kuwa Judge katika show kubwa ya TV nchini marekani, inaitwa ‘American Idol’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinaripoti kuwa J-Lo amesign mchongo huo wa kuwa Judge katika Season ya kumi ya kipindi hicho ambapo anachukua nafasi ya Ellen DeGeneres aliyetangaza kutema mzigo huo jana. Jenifer Lopez atakuwa katika nafasi hiyo ya U judge pamoja na Randy Jackson, inasemekana waandaaji walianza kumfukuzia J-Lo miezi kibao iliyopita lakini hawakufikia maafikiano mpaka wiki hii.

‘American Idol’ ni kipindi cha Luninga ambacho kinakuwa kinasaka Vipaji vya uimbaji, na tayari kupitia kipindi hicho kuna baadhi ya wasanii masuper star wametoka kupitia kipindi hicho.Kwa wakati huu J-Lo anajiandaa kuachia Album yake inayoitwa Love, ambayo ipo chini ya Island Def Jam.

Mail kutoka kwa BABA LEVO. "MAMA LEVO ANANIFANYA NIJUTE KUJIITA BABA LEVO"


Jana nilipata mail kutoka kwa msanii wa bongo fleva anayewakilisha kundi la Wanaume Halisi anajulikana kwa jina la BABA LEVO na hebu tuipitie wote.

mambo vp MZAZI?
swala hili lipo hivi. ujue mwanzo nilikuwa naona ni falaja kwa mtoto wangu LEVO kama ntatumia jina la BABA LEVO coz mwanangu akikua ataona ni jinsi gani ninavyo mpenda mwanangu.
lakini kwa sasa baada ya kuachana na mama yake. {MAMA LEVO} imekuwa tofauti kidogo coz juzi nilikuwa na show kadhaa home kwetu kigoma so wakati nipo huko ndo nikawa napata story kibao za MAMA LEVO coz amekuwa maarufu huko kwetu utazani na yeye anaimba.
na bora hata angekuwa anafanya mambo mazuri ingekuwa sio mbaya lakini daaaa!!! yaaani amefungulia geti coz hata washikaji ambao walikuwa wanamuogopa zamani coz alikuwa na mimi leo hii wamekuwa wanamnywesha mapombe wanalalanae yaani ameharibu CV yangu yoote coz kila anapopita watu wanaonyeshana huyu ndo MAMA LEVO aliyezaa na BABA LEVO ni muhuni yaaani kawa kama mtu aliyetupiwa jini la ngono sijui.
nimejiskia vibaya sana coz wakimsema yeye wananisema na mimi kwa vile hili jina ninalo litumia BABA LEVO na yeye ndo MAMA LEVO.
wanawake bana.

KAZI NJEMA MZAZI WANGU

Ni hayo tu ndugu zangu...nasubiri comments zenu je mnamshauri nini Baba Levo.