Saturday
VITU VYA KUTUSAIDIA KUONGEZA FURAHA KATIKA MAISHA YETU
1.Kujitambua na kujipenda wewe mwenyewe
2.Kuwa rafiki mzuri kwa mwenzi wako mume/mke,watoto,wafanyakazi wenzako,wazazi wako,ndugu zako,wateja wako n.k
3.Kama unafanya kazi ipende kazi yako.
4.Jivunie ulichonacho katika maisha kwa sasa na usiwe mtu wa kulalamika.Hesabu baraka zako pia.
5.Tujifunze kusamehe, tuishi bila vinyongo6.Jifurahishe mwenyewe…kwa kusikiliza muziki kama unapenda muziki ,movies,michezo mbalimbali kama mpenzi wa michezo,mazoezi n.k
7.Ijali afya yako kwa kufanya vipimo pindi unapojisikia afya yako haiko sawa,usiipuuze ili uendelee kuwa na afya njema na mwenye furaha pia.Ukiwa na afya njema utaweza kufanya hayo yaliyoorodheshwa mwanzo vyema.
8.Dini….ishike dini yako inasaidia kukupeleka katika njia iliyo sawa.
Ni baadhi ya mambo niliyojifunza nikaona sio mbaya kuweka hapa kwenye ubao wetu maana kila siku tunajifunza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment