Sunday

Mail kutoka kwa BABA LEVO. "MAMA LEVO ANANIFANYA NIJUTE KUJIITA BABA LEVO"


Jana nilipata mail kutoka kwa msanii wa bongo fleva anayewakilisha kundi la Wanaume Halisi anajulikana kwa jina la BABA LEVO na hebu tuipitie wote.

mambo vp MZAZI?
swala hili lipo hivi. ujue mwanzo nilikuwa naona ni falaja kwa mtoto wangu LEVO kama ntatumia jina la BABA LEVO coz mwanangu akikua ataona ni jinsi gani ninavyo mpenda mwanangu.
lakini kwa sasa baada ya kuachana na mama yake. {MAMA LEVO} imekuwa tofauti kidogo coz juzi nilikuwa na show kadhaa home kwetu kigoma so wakati nipo huko ndo nikawa napata story kibao za MAMA LEVO coz amekuwa maarufu huko kwetu utazani na yeye anaimba.
na bora hata angekuwa anafanya mambo mazuri ingekuwa sio mbaya lakini daaaa!!! yaaani amefungulia geti coz hata washikaji ambao walikuwa wanamuogopa zamani coz alikuwa na mimi leo hii wamekuwa wanamnywesha mapombe wanalalanae yaani ameharibu CV yangu yoote coz kila anapopita watu wanaonyeshana huyu ndo MAMA LEVO aliyezaa na BABA LEVO ni muhuni yaaani kawa kama mtu aliyetupiwa jini la ngono sijui.
nimejiskia vibaya sana coz wakimsema yeye wananisema na mimi kwa vile hili jina ninalo litumia BABA LEVO na yeye ndo MAMA LEVO.
wanawake bana.

KAZI NJEMA MZAZI WANGU

Ni hayo tu ndugu zangu...nasubiri comments zenu je mnamshauri nini Baba Levo.

No comments: