Sunday

Jennifer Lopez apata deal ya kuwa judge ‘American Idol’


Waswahili wanasema mwenye nacho huongezewa, Ana igiza, ana imba, ana dance vizuri mno, vile vile ni mjasiriamali, mpaka hapo unajua namzungumzia Nani? Namzungumzia mwanadada Jennifer Lopez uanweza muita J-Lo, pamoja na kuweza kumudu mambo hayo yote niliyoyataja, hivi karibuni amesign deal ingine kali ya kuwa Judge katika show kubwa ya TV nchini marekani, inaitwa ‘American Idol’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinaripoti kuwa J-Lo amesign mchongo huo wa kuwa Judge katika Season ya kumi ya kipindi hicho ambapo anachukua nafasi ya Ellen DeGeneres aliyetangaza kutema mzigo huo jana. Jenifer Lopez atakuwa katika nafasi hiyo ya U judge pamoja na Randy Jackson, inasemekana waandaaji walianza kumfukuzia J-Lo miezi kibao iliyopita lakini hawakufikia maafikiano mpaka wiki hii.

‘American Idol’ ni kipindi cha Luninga ambacho kinakuwa kinasaka Vipaji vya uimbaji, na tayari kupitia kipindi hicho kuna baadhi ya wasanii masuper star wametoka kupitia kipindi hicho.Kwa wakati huu J-Lo anajiandaa kuachia Album yake inayoitwa Love, ambayo ipo chini ya Island Def Jam.

No comments: