Sunday
Nicki Minaj akanusha album yake Kuleak
Young Money member Nicky Minaj amewahakikishia Rap Fans kuwa ngoma iliyoleak kwenye Internet kuwa haipo kwenye album yake anayotarajia kuiachia mwishoni mwa mwaka huu. Akiwaandikia followers wake wanaokadiriwa kufikia milioni moja katika mtandao wa Twitter, jana mchana Nicki Minaj alikanusha ku leak kwa album hiyo. Amesema ngoma iliyo leak ni ya zamani. Pia mwanadada huyo akasema Video ya ngoma yake itakuwa kwenye iTunes hivi karibuni. Kama unakumbuka Mshkaji wake wa karibu Drake aliwahi kupatwa na balaa la kuleak kwa album yake ya Thank me Later, na kitu kama hicho huweza kusababisha mauzo ya album husika kutokufanya vizuri wakati itakapotoka. Nicky anatarajia kutoa album yake Novemba 23 mwaka huu, bado hajaipa jina na wakati watu wanasubiri atoe jina basi waiite Nicki Minaj: The album.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment