Thursday
KUTANA NA WATU WAPYA,INASAIDIA.
Kwa walio wengi kukutana na kupata nafasi ya kujua watu wapya ni raha sana.Ila kuna wengine huona ni kupoteza muda,hujisikia hayuko huru hasa kama huyo mtu anamuuliza maswali au kumuongelesha.Ila kuna faida kubwa ya wewe kujipa nafasi ya kukutana na kufahamiana na watu wapya mara kwa mara.
Urafiki..
· Kukutana na watu wapya kunaweza kukuongezea marafiki.Hali ambayo inakusaidia kiakili na kimwili .Mtu mpya anaweza kukufundisha kitu kipya ambacho wewe ulikuwa hujui,kukupeleka mahali ulikuwa hujawahi kwenda,kula chakula ambacho ulikuwa hujawahi kula n.k
Kujifunza
· Kukutana na watu wapya kunakusaidia kujifunza vitu vipya.Ukikutana na mtu mpya utajifunza vitu vipya,mbinu mpya za kufanya jambo fulani,lugha mpya,au kuweza kukupa njia ya kutatua tatizo Fulani kwenye maisha.Ukichukua muda kumjua mtu inaweza kukusaidia kuongeza wigo wako wa ufahamu na kujua mbinu mpya katika maisha.
Uelewa
· Kukutana na watu wapya kunakupa nafasi ya kuelewa tamaduni tofautitofauti imani,wanavyoishi,wanachothamini pia.Unaweza jifunza mfumo wao wa kisiasa,makabila na dini.
Kikazi/kibiashara
· Ukikutana na watu wapya unaweza kupanua wigo wako wa kibiashara kwa kupata connections mbalimbali .Pia hakikisha unangalia huyu mtu mpya anaweza kufanya nini katika kazi yako na wewe kufanikiwa, na hata wewe unaweza kumfanyia nini pia kwake.
Kujiamini na kujisikia vizuri
· Kukutana na watu wapya kunakusaidia kujisikia vizuri wewe mwenyewe.Ikitokea mtu mpya anaonekana kuvutiwa na wewe na maisha yako kiujumla unasikia kabisa kuna kitu kinakupa faraja.Kama ulikuwa upo katika wakati unajihisi huna thamani huwezi jua mtu mtu anaweza kukufanya uanze kuona thamani yako.
Kutana na karibisha watu wapya labda kwenye hafla mbalimbali za kiofisi na kibiashara,mikutano,kwenye harusi,sherehe,hata msibani,kwenye stand,kwenye burudani mbalimbali..yaani inaweza tokea popote pale.
MUHIMU
Usiweke sura ngumu tabasamu,tabasamu lina nguvu sana hata kama hujaongea chochote inamfanya mtu asiogope kuanzisha maongezi na wewe,inasaidia sana hasa kama upo mahali kuna mkusanyiko wa watu kama kwenye mikutano,sharehe,starehe,na haumjui yoyote.Lakini ukiweka sura ngumu utashangaa unarudi nyumbani hujamfahamu yoyote maana mtu anakutazama anaona mmh huyu si mtu rahisi kuanzisha urafiki nae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment