Wednesday
ALIYEJIFANYA MENEJA WA DRAKE KIZIMBANI
Jamaa mmoja kutoka Milwaukee, Wisconsin nchini marekani, anashtakiwa kwa kujipatia pesa kinyume cha sheria, na hiyo ni baada ya kujifanya yeye ni manager wa Lil Wayne na Drake. Kwa mujibu Document za shtaka lililofunguliwa na kampuni Eagles Intertainment Inc, inasemekana mshtakiwa Joey Turner Jr. a.k.a Jo Flowrushus, alijifanya yeye ni Cortez Bryant ambae ni meneja wa Drake so ana mamlaka ya kusimamia booking zote za Drake.
Joey Turner aliwasiliana na Eagle Intertainment kwamba Drake anataka Dola elfu 90 kwa ajili ya show, na kampuni hiyo ilitoa Dola elfu tisa kama Deposit ya show hiyo ambayo ilitakiwa kufanyika tarehe moja Septemba, katika miji wa Milwaukee Wisconsin. Kesi ipo mahakamani, na Kampuni ya Eagle Intertainment inataka ipewe
Na mtuhumiwa dola elfu 27, kufidia gharama za kumlipa mwanasheria na gharama ya kufungua kesi hiyo mahakamani. Kampuni inayohusika na bookings za Drake ni International Creative Management pekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment