Thursday
INAPOTOKEA UMEALIKWA CHAKULA NYUMBANI KWA NDUGU,RAFIKI AU JAMAA ZINGATIA YAFUATAYO.
1.Usitoe comment mbaya kuhusu chakula unachokula maana kuna mtu amejiandaa sana kupika hicho chakula .
2.Usiongee ukiwa na chakula mdomoni
3.Onyesha kufurahia chakula
4.Kama unahitaji kitu kama chumvi,bakuli ya mboga au chochote na haufikii omba usogezewe na sikupitisha mikono kwa mwenzako ambae tayari anakula.
5.Usitoe kitu mdomoni ukakiweka juu ya meza,kama ni mfupa toa mdomoni weka pembeni kwenye sahani yako.
6.Usibeue/kutoa gas kwa sauti...
7.Ukialikwa mlo kwa rafiki,ndugu au jamaa baada ya mlo shukuru na ueleze ni namna gani umefurahia chakula ulichokula unaweza ukasifu mboga kwa mfano labda "samaki alikuwa mtamu kapikwaje maana kama sijawahi kula samaki.."
na mengineyo tunaweza kukumbushana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment