Thursday
Maisha jinsi yalivyo sasa hivi hatuhisi kwamba mtoto wa kiume anatakiwa kuandaliwa kuishi na mtoto wa kike wa kisasa?.Zamani mtoto wa kike alikuwa alikuwa anaandaliwa mapema nyumbani namna ya kuwa mke wa mtu na majukumu ya kifamilia.Lakini kwa sasa mtoto wa kike anahimizwa kuhusu suala la shule kwanza,kazi nzuri,na mwisho kabisa ndio kuwa mke mtarajiwa.
Msichana huyu anapokuja kukutana na mtoto wa kiume kuanzisha familia wote watakuwa na sauti,mwanaume akiongea ujinga mwanamke atamkosoa kwamba hapana hapo sio hivyo ni hivi.Na pia kwa muda kumekuwepo na ile hali ya wanaume kuogopa wanawake wasomi kwa sababu wanasema wanajifanya wajuaji.Ila kwa sasa imefika wakati mwanaume pia atambue kuwa kuwa na mwanamke msomi sio kukaliwa kichwani hapo ndipo tunahitaji kumuandaa namna ya kuishi na mtoto wa kike wa kisasa...shule kwanza,kazi,halafu ndio kuishi na mume.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment