Mkali
wa RnB Tanzania ambaye kwa sasa anaendelea kula matunda ya ndoa,Joseph
Kelvin Mapunda aka Q-Jay kwa sasa ameokoka na kuamua kumfuata yesu!
Q-Jay amekuwa akitolea nje concert kibao ambazo anaalikwa kwa ajili ya
kufanya show,kutokana na imani yake mpya aliyonayo sasa,na amefunguka
kuwa “mziki niliokua nafanya ulikua ni wa dunia na ningewashauri
wasanii wenzangu wote wanaoimba nyimbo za dunia kuufata wokovu na
kuachana nazo,kwa sasa nimepumzika kufanya shughuli za mziki lakini
kuanzia mwezi wa sita nitaanza kurekodi mziki yangu mipya ya
kumtukuza mungu yaani gospel na natarajia kutoa
album”....alimalizia Q Jay kwa sauti pole ya kilokole,akifuata nyayo za
Stara Thomas,K Basil na Renee Lamira!
....ENZI ZA WAKALI KWANZA...Q-JAY NA MAKAMUA WAKIFANYA MIZIKI YA KIDUNIA!
Q-Jay
alianza 'muziki wa kidunia' akiwa na kundi la RnB,Wakali Kwanza na kina
Joslin,Makamua na wengine kibao na mara ya mwisho walitoa album ya
pamoja na Makamua wakiwa chini ya MJ Records na nyimbo zake za kidunia
kama Sifai featuring Joslin,na collabo kama Kitu Gani,Nakupa Sifa
alizinukisha vilivyo
No comments:
Post a Comment