Thursday
The good dr, dr dre, ahaidi kudrop album yake ya detox kama zawadi ya christmas kwa mafanz
Album ya detox ya dr mwenye degree ya kitaa ya kugonga midundo heavy, mzeiyah dr dre, imekuwa kama stori za popo bawa…..hujui uamini lipi kuhusu stori za ujio wake lakini for now gwafara hot of the gwafa-press ni kwamba akiwa katika uzinduzi wa toleo lingine la headphones chini ya nembo ya beats by dre jijini new york, duka la best buy………..the good daktari dre, amelonger kwamba yupo katika nafasi nzuri ya kuahidi kwamba album hii ambayo imemchukua miaka kumi kuikamilisha itadrop chrismasi hii ya 2010
Mwenye kiti wa interscope, label ambayo dre anafanya kazi chini yake, mzeiyah jimmy lovine amesema wao wanampa dre support asilimia elfu mmoja ili kuhakikisha kwamba album inadrop on Christmas day mwaka huu!!!
Dre analonger longer kwamba amekuwa anerekodi kila siku na kikubw aanacho hofia ni kutoa mzigo ambao mafanz hawataupenda ndio maana kila siku anarekebisha hiki au kile……
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment