Thursday

A.Y Atoboa Siri ya Kupiga Collabo na Wasanii wa Kimataifa


Baada ya kupiga Collabo na Miss Trinity katika studio za B-Hits, weekend hii Ambwene Yesaya a.k.a A.Y amefichua siri ya kupiga Collabo na Wasanii mbalimbali wa kimataifa wanaoshuka bongo kila kukicha. A.Y ameyasema hayo baada ya kuulizwa na swali na dawson kwamba ni mbinu gani anayoitumia katika kumshawishi mtu kama Sean Kingston, P-Square, Miss Trinity, K-Naan na wengineo.

Ambwene akajibu kuwa siri yake ya mafanikio hayo ni kujitangaza sana kupitia vyombo mbalimbali vya habari kadri inavyowezekana, so anapokuja msanii kutoka nje Tayari wanakua wameshafanya utafiti wa kujua ni msanii gani mkali au anayejulikana nchini Tanzania.

Ambwene pia amezungumzia Collabo yake na Sean Kingston ambayo walishindwa kuifanya hapa bongo na meneja wa Kingston akamshauri Ambwene kuwa ili aweze kujitangaza zaidi ni bora aende kurekodi nchini marekani kwani atapata fursa ya kukutana na wataarishaji wa muziki wa kimataifa lakini pia kazi atakayofanya na Kingston itakua yenye ubora.

A.Y yuko mbioni kwenda katika mji wa Miami nchini marekani kurekodi ngoma na mtu mzima Sean Kingston.

Lakini pia kesho A.Y anaelekea jijini Kampala kupiga Video ya ngoma aliyorekodi na Miss Trinity.

No comments: