Thursday

Wyclef Cleaf Jean Akanusha Kuwania Urais Haiti


Wyclef Jean amekanusha uvumi uliokuwa ukimhusisha na kugombea uraisi nchi Haiti, Hivi karibuni sehemu mbalimbali ulimwenguni hasa nchini marekani na Haiti, kulienea Taarifa za kuwa Wyclef Jean anajipanga kushiriki katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini Haiti mapema mwezi Novemba mwaka huu. wakati akifanya mahojiano na mwandishi mmoja hivi karibuni ambapo alitakiwa kueleza ana nia ya kuwania urais.

Wyclef alijibu kama ifuatvyo: " kama ningekua nimeamua kugombea ningekuambia lakini ninachoweza kusema sasa hivi ni Nooo"

Pamoja na Wyclef kukanusha uvumi huo, lakini kuna taarifa zinasema mtu mzima yupo nondo vibaya mno, na tayari amepanga Vichwa vikali vya wasomi ambapo kazi yao ni kumshauri nini cha kufanya wakati wa Kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Raisi wa Haiti. Wiki ya kwanza ya mwezi wa ujao wa nane ndo kila kitu kitajulikana kwani ndo itakuwa Deadline ama wiki ya mwisho ya kuchuka fomu za kuwania urais so tutajua Kama Wyclef mtoto wa Jean kama atagombea ama hatagombea U president katika Taifa hilo maskini. coz akienda tu kuchukua fomu au kurudisha, Paparazi wanamsubiri na Camera zao.

Kupitia Taasisi yake ya misaada, Wyclef amewahi kusimamia uchangiaji wa Dola milioni kumi za kimarekani kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi nchini Haiti, Tetemeko ambalo lilipelekea vifo vya watu zaidi ya laki tatu na kuacha mamilioni ya watu wakiwa hawana makazi.

So hiko ni kigezo cha watu kumpatia kura za kutosha jamaa.

Sipati Picha Mr. President Wyclef Jean pale kati ameapishwa, sijui ataacha music? ajja jja jja jja jjaaa.....

Tags: Akanusha, Cleaf, Haiti, Jean, Kuwania, Urais, Wyclef

No comments: