Thursday

CONCERT YA RAPPER NELLY YAWEKEWA MIZENGWE MAREKANI


Show ya kwanza ya Rap iliyopangwa kufanyika katika mji mdogo wa Branson, Missouri nchini marekani imeingia kwenye utata na maofisa wa mji huo. promota wa Concert hiyo Paul Dunn alitaka show hiyo ipigwe katika sehemu ya Parking ya ukumbi wa The Grand Palace kutokana na ukumbi huo kufanyiwa matengenezo kwa ndani. Parking hiyo inauwezo wa kuingiza watu 6000 wakati ndani ya ukumbi huo kunaweza kuingia watu 4000.

kwa mijibu wa chanzo chetu cha habari kinasema kuwa mkurugenzi wa mipango miji wa Missouri amechomoa ombi la waandaaji wa Concert hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo makelele, Parking, na udhibiti wa watu watakao kuwepo siku hiyo. Mkurugenzi huyo pia amelalamika kuwa waandaaji wa Concert hiyo wanaendelea kupromote kuwa mtu mzima Nelly atapanda katika stage tarehe 21 August na pia tayari wameanza kuuza ticket za onyesho, huku wakitambua bado makubaliano hayajafikiwa.

Waandaaji wa Concert wamesema wanashangaa kuulizwa maombi mapya wakati tangu awali walishapeleka maombi, jamaa wanampango wa kukata rufaa kwa board ya jiji. Rufaa ya waandaji itaambatana na vielelezo vya mpangilio wa ulinzi utakavyo kuwa siku hiyo, pamoja na Documents zenye Signature za majirani wa eneo husika, wakithibitisha kuwa wao majirani wamebariki Concert hiyo kufanyika Branson.

inasemekana concert hiyo itaingizia mji wa Branson mapato ya dola za kimarekani laki tano.

Inawezekana uongozi wa mji huo unabana mchongo kwa sababu za kihistoria kwani mji wa Branson ni mji flani uliopoza na pia kipindi cha nyuma asilimia kubwa ya wakazi wake walikuwa ni wapenzi wa Country Music, hata wakongwe wa mziki wa Country nchini marekani kama Kenny Rogers, Wyne Newton na Pat Boone wanaishi Branson.( Yaani pamoja na muziki wa Hip Hop kuanza miaka mingi nchini marekani lakini wakazi wa mji wa Branson hawajawahi kushuhudia mwanamuziki wa Hip Hop akikanyaga jukwaa lao hata siku moja) Aiseeeee.... Dar es salaam wamekuja Rapper wangapi kutoka nchini marekani? Jiulize?

hata sisi tunawashinda Branson, na huku ni Thousands of miles....

Kwa mujibu wa waandaaji wa Concert tayari mashabiki elfu tatu wamekwisha nunua Ticket ili Kumshuhudia Mtu mzima Nelly na kundi lake la Saint Lunatics wakishusha swager za Hip Hop kwa mara ya kwanza ndani ya mji wa Branson

No comments: