Monday
Posted by DINA MARIOS at 10:53 PM 0 comments JAMANI! TUWE TUNASOMA UJUMBE MARA TUUPATAPO!!!
Mchungaji akiwa katika pitapita zake za kuombea katika wodi za hospitali fulani, akakuta kuna Mgonjwa aliekuwa hawezi kuongea japo alikuwa na fahamu na aliwekewa oxgen. WAKATI AKIOMBEWA, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, Akaandika haraka haraka na akampa yule Mchungaji. Ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO. Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema; "KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA" Akampa mmoja wa wanandugu akisome. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa: "UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment