Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata zaidi ya wasichana wapatao 22
eneo la Mwananyamala karibu na geti la Mwananyamala hospitali akiwemo
mama mtu mzima anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye alikuwa
anamiliki jumba lenye zaidi ya vyumba 40 ambalo utumika kufanyia ukahaba
maarufu kama danguro.
Akitoa taarifa leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
Kamanda Charles Kenyela, alisema kuwa wanashukuru wananchi ambao
wameweza kutoa ushirikiano wa kukamatwa kwa wasichana hao ambao walikuwa
wakifanya biashara ya ukahaba katika maeneo hayo kwa muda mrefu.
Mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa wanalishukuru sana Jeshi
Polisi kwa kuweza kuwakamata wasichana hao ambao wamekuwa wakifanya
biashara hiyo ya ukahaba kwa muda mrefu.
"Tunalishukuru sana Jeshi la polisi kwa kuvunja kero hii ambayo
imekuwa ikitukera tokea muda mrefu sana, yani danguro hili lipo tokea
mwaka 1990, mimi nazaliwa nalikuta mpaka leo lipo ila leo ndiyo polisi
wamekuja kuwakamata wahusika" Alisema mmoja ya vijana wanaoishi eneo
hilo.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa wanafanya biashara
hiyo kwa bei ya shilingi 2000, 3000 kwa muda mfupi (short time) na
wateja wao ni vijana, akina baba pamoja na vijana ambao huwa wanabarehe
kwa vile hawa huwa hawajui mapenzi huko huenda kufundishwa...
No comments:
Post a Comment