Sunday

STAR MEAGAN GOOD ALISHAWEKWA NDANI MUDA MREFU..




Hatimaye nyota wa filamu ya Think Like a Man Meagan Good amefunga pingu za maisha na mhubiri na makamu wa rais wa Columbia Pictures DeVon Franklin juzi huko Malibu, California nchini Marekani.
Good, 30, na Franklin, 33, walitamka ile sentensi maarufu “I do” katika eneo la Triunfo Creek Winery mbele ya wageni 400 akiwemo Derek Luke, Tracey Edmonds, Deion Sanders na Tasha Smith.
Good ameliambia jarida la People, “DeVon hunifanya niwe bora, hujaza maisha yangu na hukamilisha ubora wa maisha yangu. Yupo kwenye timu yangu nami nipo kwenye yake. Mungu ameufunua moyo wangu kwake kuliko mtu yeyote.”
Naye Franklin alisema, “Sijawahi kuwa na amani na furaha hivi kuliko nilivyokuwa naye.”
Good na Franklin walikutana kwa mara ya kwanza miaka sita iliyopita wakati wakijadiliana kuhusu project ya filamu.
Good ni dada yake na mwanamuziki Lamyia Good aliyeshirikishwa na AY kwenye wimbo ‘Speak With Your Body’.Huwa nampenda huyu mdada mpaka upendo wangu umepitiliza nahisi wivu kwa De Von...

1 comment:

Anonymous said...

hahahahahahah....
There iz nathing u kan du rather than
Buyin her projects..
Otherwze sTaY awaY from heR Yang bwoY!
....she aint urs enmore//: