Thursday

LEO 1.Kila siku ni siku ya kujifunza jambo jipya iwe kwa kusikia,kuona au kupitia katika maisha. 2.Kuheshimu wengine. 3.Kuacha uoga,wengi wetu tuna uoga wa kufanya jambo fulani.Mfano kusimama na kuongea mbele za watu na mengine.Pambana na huo uoga pengine unakunyima nafasi ya kukua katika kujiamini. 4.Kujipenda mwenyewe kwanza. 5.Kuwapenda na kuwajali wengine wote wanaokuzunguka haijalishi upungufu walionao. 6.Kuwa mpenzi mwenye kukidhi mahitaji ya mpenzi wako.Ikiwemo kuwa mwaminifu,mkweli,kujali,kumheshimu mwenzako n.k 7.Kuwa mtu mwenye kusamehe. 8.Acha kulalamika juu ya matatizo yako,yafanyie kazi. 9.Tambua thamani yako. 10.Jishauri wewe mwenyewe,wakati mwingine huwa tunaomba ushauri kwa watu wengine huku tukiwa na majibu sahihi ndani ya mioyo yetu. Kwa leo ni haya tu japo yapo mengi.

No comments: