Tuesday
Askari achunguzwa kwa kumpendelea Wayne garezani
Mlinzi katika Gereza la Rikers huenda akawajibishwa kutokana na kumpa huduma za upendeleo Super mfungwa katika gereza hilo, Rapper Lil Wayne.Uongozi wa Gereza hilo umeanzisha Uchunguzi dhidi ya Captain Brown baada ya kupokea malamiko kuwa mlinzi huyo anaspend extra time na Lil wayne.
Gazeti la New York Post linaripoti kuwa Captain Brown alikua akimruhusu Wayne kukaa kwenye Cell yake wakati wafungwa wenzake wakiwa wameamriwa kwenda Recreation Yard(kufanya shughuli nyingine)
Mlinzi alisahau kuwa wafungwa wote wanapokua gerezani wanakua ni sawa. Mapema mwezi wa nne mwaka huu, mwezi mmoja tu baada ya Wayne kuingia katika gereza hilo, Amelia Negron mlinzi katika gereza hilo, alifukuzwa kazi kutokana na kumspy Wayne kinyume cha sheria.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa Walinzi wa gereza hilo kukutikana na hatia ya kuwapendelea Masuper Star wanaofungwa katika gereza hilo, Mwaka 2009 kuna ripoti ya uchunguzi ilithibitisha kuwa Foxy Brown alikua akipata huduma za upendeleo wakati akitumikia kifungo cha miezi tisa katika gereza la Rikers mwaka 2006.
Inasemekana foxy Brown alikua akipata huduma za kutumia simu na kuwatch Tv bila ukomo, alikua akipata Make up, Nguo za gharama na chakula kutoka nje
October 2009 muhusika yaani mlinzi huyo aliresign kuokana na Scandal hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment