Friday
ALI KIBA ATEMANA NA MENEJA WAKE WA SIKU NYINGI (G-Lover)
Hivi karibuni tulipata taarifa kuwa Msanii maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya Ali kiba, ametemana na Label ya G-Records na kuamua kufanya kazi kimpango wake, Tulimtafuta Ali Kiba ili athibitishe taarifa hizi….na kumuuliza je taarifa hizo ni za kweli: ALI KIBA alithibitisha hilo, na kusema ameamua kumpunguazia majukumu bosi wake wa zamani/G-Lover kwani anahisi yupo busy sana na kazi zake za kuongoza kituoni flani cha radio kilichopo visiwani zanzibar, nilitaka kufahamu amejiandaaje na safari ya kimuziki huku akiwa mbali na mtu aliyemuongoza kuanzia under ground level mpaka hapo alipo? ali kiba alijibu kuwa ameshazoea kwani ni siku nyingi alishaanza kujiongoza kwa msaada wa kidogo wa g-lover.
haikuishia hapo, tuliamua kumtafuta mtu mzima G naye akathibitisha hilo, na kusema kuwa hawana ugomvi wowote na Kiba, kilichopo wakati huu kama kiba atataka kurekodi katika studio yake basi atatakiwa kulipia kama wasanii wengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment