Hebu tujadiliane hili; Unaishi jijini Dar es Salaam, unaye mpenzi wako ambaye unampenda sana. Huyo alikuwa akiishi mkoani Mbeya, lakini amekuja Dar kama wewe kutafuta maisha. Mkakutana na kupendana, baadaye mkaamua kuanza kuishi pamoja.
Lakini unaye rafiki yako kipenzi, ambaye unamuamini na kumuheshimu sana. Mara nyingi amekuwa akija kukutembelea nyumbani jioni na mnashiriki pamoja chakula cha usiku mara nyingi. Siku moja ukiwa ofisini, unagundua kwamba kuna kitu ulikishau nyumbani, unaamua kurudi kwa ghafla.
Ile unaingia sebuleni, unashangaa kukuta nguo za mwanaume pamoja na viatu, ulipoenda chumbani, unamkuta mpenzi wako yupo utupu na rafiki yako, wakiwa katika maandalizi ya kufanya mapenzi.
Pambanua ubongo wako. Kama ni wewe utachukua hatua gani? Tujadiliane.href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEvIyewWAPj7_OnDSHfwtjHjAbFi9PSEg6-h794f714mHRtu8h9PSm0HfJWRJ1tVz1g8QvjvyiQGAqviKHQ6QARck0tZi9GbKX_lNVCgOg1coUHH0fy-VYTOQCiITLQyx0gsE3b4-eyd4/s1600/mahabaa.jpg">
2 comments:
Kama sijamwoa kiukweli namwacha kabisa.
Kiukweli nikumwacha tu kwann amekubali kupigwa na mchz tena room kwangu.
Post a Comment