Tuesday
MPENZI WAKO ANAPOACHA KUJIBU SMS ZAKO, ANAMAANISHA NINI?
Hi, marafiki! Muda kidogo nilikuwa sipo, mambo yanabana sana, lakini leo nimeamua kurudi. Naanza na hili, mpenzi wako anapoacha kujibu meseji zako unamchukuliaje?
Iko hivi, wapenzi wengi wanapenda sana kupewa nafasi ya kwanza kwa kila kitu, hakuna ubishi wapo sahihi na wana haki ya msingi kabisa!
Hebu vuta picha, fikiria kwa makini, unaye mpenzi wako, ni mchana upo kazini, upo busy sana, lakini ukakumbuka kuwasiliana naye japo kwa sms ya kichokozi tu; "Hi sweet, are u ok? Umekula nini leo? Luv u..." ukaituma kwa mwenzi wako.
Tena sikia, baada ya mpenzi kutuma sms ya love kama hiyo ambayo hasa inakuwa inamu-wish mlo mwema, anakuwa anasubiri majibu yake kwa hamu kubwa sana, lakini giiiii....hakuna majibu wala ma-answer.
Unadhani nini kinasababisha hili kutokea? Na kama ungekuwa wewe umetuma sms kama hii kwa mwenzi wako, halafu hajajibu, unachukuliaje?
Weka maoni yako, halafu nitakuja na tip zangu, nitakuwambia nini husababisha na nini cha kufanya ili kuweza kumjua mwenzi wa aina hii.
Karibuni tuchangie...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
4 me i concider may be hana hela,but nikimpa credit hajibu mtamuuliza why dis then akijibu ntajua chakufanya kutokana namjibu yake.
Dawa ya demu km huyu nikumpigia phone then utajua km kachuna au nimkwanja umekata kwenye phone.
Post a Comment