Tuesday
UNAKUMBUKA STORY HII YA BABA WA MUSIC
Ukiachilia mbali suala zima la kutupia ulimi pale kati, mixa ming’aro ya ziada kiasi cha kumpiga jeki yule asiyekuwa na mauzo ya kutosha…. Leo namdondosha kwenu ‘HANDSOME’ ambaye yeye binafsi anaamini anashine bila bling bling kwasababu ana Mwili na Sura nzuri na hii ni tangu enzi za analogi hadi digito (SWAGGA)
Anaitwa Dully sykes au Prince Dully sykes a.k.a Blazameni Dully a.k.a Mr Misifa ambaye ametuibukia pande hizi ili kuturimaindi kuhusu Historia ya huu mziki wetu wa Bongo Flava.
Huyu Blaza alianza Muziki miaka ya 1994 kipindi cha akina Saleh Jabir, naposema kipindi cha akina Salehe Jabir namaanisha ni enzi zile wasanii wetu wanachukua nyimbo za nje na kuzitafsiri kwa kiswahili.. ni kipindi ambacho kilifuata baada ya kile cha ‘MIE NI MSELA/ NINA KICHWA KAMA PERA/SIWEZI KWENDA JELA/ KWASABABU NA MAHELA…’3 Bila shaka hiki ni kipindi ambacho Ubunifu ulikua umeanza kupewa kipaumbele, naam, hii ni hatua ya 3 baada ya ile ya kuimba nyimbo za nje kama zilivyo, kipindi hicho tulikuwa na wakavaji (hawa ni wale ambao walikua wakiipenda ngoma tu lazima waikariri na waifanye kwenye show zao) so tukawa na vikundi vya Naughty by nature wabongo, Michael Jackson wa bongo, Mc Hammer wa bongo na Vannilla Ice wa Bongo.
Elvis,Michael Jackson,UB 40, ni baadhi ya wale waliomuinspaya(kumvutia kimuziki) huyu Prince wa Bongo Flava.. na alikua akiimba nyimbo zao na kuzicheza kama wao kwenye maafali ya darasa la saba au birthday parties za mitaa yake ya kariakoo, show yake ya kwanza ilipigika ndani ya shule ya Shaaban Robert mnamo mwaka 1996 na huko aliwaambia INFORMER ya SNOW,na Dj alikua P FUNK kutoka shule ya IST (International school of Tanganyika
Dully alipenda kuwa Mwanamuziki mwenye nyimbo zake mwenyewe na sio zile za kuiga,na katika kulikwepa hilo alijitengenezea utaratibu wa kuandika nyimbo kwa kufuata hisia zake yeye mwenyewe kama yeye,kwahiyo hakuwa na jinsi zaidi ya kuibuka maeneo ya studio za Don Bosco mnamo mwaka 1998.
Hata hivyo juhudi zake za kurekodi nyimbo Don Bosco ziligonga Mwamba baada ya kukuta foleni kubwa pale studio na zile nenda rudi za Maproducer wetu.. ‘waliniambia niwalipe Elfu Tano ili nirekodi..na hiyo ndo ilikua bei kamili ya studio, nikawapa na pia kama haitoshi nikanunua hadi Chrome.. tatizo studio ilikua bize halafu mie nilikua na mizuka ya kutosha so sikutaka kuwapa pointi, inshoti niliwapotezea lakini hadi leo ile loss ya ELfu Kumi inaniuma.. © Dully
Judgement day(ilirekodiwa Marimba records chini ya Mpishi Mr Chaz) ndo title ya Ngoma yake ya kwanza,kwa bahati mbaya haikufanya vizuri kabisa, hakuna aliyeikubali au kuielewa.. lakini siku zote mwanzo huwa mgumu au vipi? Well,hakuna asiyejua ya kwamba Hustla huwa hachoki kwasababu Nia ya mtu huwa imo ndani ya dhamira yake, so ni yeye wakuitengua au kuitilia mkazo
Dully aliamua kujifanyia research yeye mwenyewe ili akijue kile kilichosababisha Tonge lake lisifike Mdomoni na kabla Udhaifu wake haujamulemea,alibahatika kukutana na Dj Stevie B au ‘SKILLZ’(kitambo hicho alikua anaswagua pale Sugar ray) desemba ya mwaka 99 na ushauri pekee aliopewa ni ‘UNAIMBA VIZURI TATIZO WABONGO WENGI HAWAJUI KIINGEREZA, NADHANI UTAFIKA HUKO UNAKOTAKA KWENDA KAMA UTATUMIA KISWAHILI KWENYE TUNGO ZAKO MDOGO WANGU’
Unajua ukweli huwa unahitaji maneno machache tu, nadhani ndo maana ikaclick fasta kwenye ubongo wa mwanafleva huyu na kabla ya karne ya 21 kuingia tayari alikua ashakutana na Mika Mwamba na kile kibao cha ‘JULLIETTA’ kilitoka na kumtambulisha vyema kwenye Medani ya Mziki.
Bila shaka ukimuuliza Mwanamuziki yeyote ambaye anatamba hivi sasa au ashawahi kutamba kuhusiana na hizi chati zetu za kibongo atakuambia ‘kuhiti sio vigumu,vigumu ni kupakua hits baada ya hits’
Ujio wa Dully Sykes ulikuwa ni wa kipekee,bora na wa maana kabisa na cha kushangaza zaidi ni pale alipoongeza makakamavu na kuziacha sifa zimjenge badala ya kubweteka na ktk kulithibitisha hilo aliendelea kupakuwa mawe ya nguvu kama 1- stori ya ukweli 2- Nyambizi 3- Mr Misifa (alipewa na P Funk hilo jina) 4-Salome
Mwaka 2002 alizindua album yake ya kwanza pale Diamond Jubilee, na uzinduzi wake uliendeshwa kwa style ya NANI ZAIDI?kati yake na T.i.d (Top in Dar) na mpaka tunarudi mitamboni ukumbi mzima ulikua upande wa Dully na hali hio haikunishangaza hata mimi kwasababu kazi za Dully zilikua sio kama zile za KOBE WA JUU YA MTI,yaani hapa namaanisha sio mpaka apandishwe ndo awe juu,so tayari mshajua nani alionekana kidume siku hiyo au vipi? Naomba tukumbuke ya kwamba style hii ya kuwapambanisha Magwiji hawa ilitumika kama njia ya kuwavutia mashabiki, kuwapa hamasa ili wajitokeze kwa wingi ukumbini na wala sio kama hawa jamaa walikua na Bifu kama ambavyo wengi walifikiri hapo mwanzoni au labda minong’ono ya nani mkali Mitaani.
Dully aliendelea kulitetea Taji hilo la Mkali wa Bongoflava kwa kupakuwa Mawe mengine ambayo yote yalihit au bado yanasumbua kwenye chati kama 1-Handsome 2-ladies free 3-kijakazi 4-hi 5-leah 6-tanita 7-Jackie 8-Eva 9- Rafiki 10-Latoya 11-Nakupenda 12-Ningejua 13-Mariah Mariah 14- Bijoux 15- hunifahamu 16-Loudspeaker 17-asha Mapromise 18-Baby Candy 19-Watasimuliwa 20-Miss Tz UK 21-Dhahabu 22- dully’s Chick 23-Kupenda 24-Malaika 25- Tamika 26-Opalina 27-Monalisa 28-Sikutaki tena 29-Papa 30-Tata 31-Shikide (ambayo inahit hivi sasa)
Uandishi wa nyimbo zake haupo kwa ajili ya kukufanya ufikirie sana ili kuelewa kile alichokiimba na uimbaji wake ni kama anafanya Mzaha hivi au unaweza sema hayuko serious lakini ukimtegea sikio zaidi utagundua nia na madhumuni yake ni kukufanya uburudike kwa kupitia sanaa yake na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka kama alivyosema Shaaban Robert, ni ukweli Dully Sykes anasifika kwa kuimba Nyimbo zenye ujumbe mwepesi na nyingi zikiwa ni za mapenzi au kujisifia yeye ni nani lakini ni nyimbo hizo hizo ndo zimemfanya akubalike na pia ninathubutu kusema ni aina ya Nyimbo ambazo Jamii inazielewa na kuzipandisha chati mapema zaidi kuliko zile za ki-u-wanaharakati.
VITUKO.
(1) Sote tunajua Chura anayapenda Maji lakini sio ya moto vivyo hivyo Dully anapenda sifa lakini isiwe na dharau ndani yake, moja kati ya matukio anayoyakumbuka ni pamoja na lile deni la shilingi mia moja ya kitanzania aliyokopeshwa na Mdau mmoja wa kitaani kwake kwa ahadi ya kuirudisha pindi tu akitoka au kufanikiwa kimziki… ‘unajua hakuna kitu cha bure sikuhizi,right?nakukopesha hii shing mia ya nauli leo, lakini naomba if utafanikiwa kimziki unirudishie shing mia yangu… ©Mdau
(deni hilo lilipwa tena kwa kiasi hicho hicho cha fedha miaka mitatu baadaye na hiyo ilitokana na yeye Dully kuwa bize na show nyingi za mikoani)
(2) Anasifika kwa kulamba lipsi zake na pia anahisi wasanii wengi wa bongo fleva wakiongozwa na Yule star wa mmarekani wakuitwa LL COOL J wanamgeza yeye Dully Sykes kulambalamba lipsi zake.
(3) Yeye ni mtu wa kwanza kuleta masuala ya Camp, (alipokuja na Misifaz Camp baada ya kuchoshwa na zile stunt za ZERO BRAIN) anajivunia kwa hilo na kwa upande mwingine anasikitika kwasababu ni Camp hiyo hiyo ndo iliyozaa na kulea asilimia kubwa ya Madansa na pia ni Misifaz Camp hiyo hiyo iliyosababisha watoto wa dogo watoboe masikio yao na kuyavika hereni au kujipiga tattoo kabla ya kuwauliza au kupewa ruhusa na wazazi wao, na pia ni Camp hiyohiyo iliyosababisha asilimia kubwa ya Madansa waashie shule za msingi au hata kufukuzwa wakiwa darasa la tatu na kuendelea.
(4) Msanii wa kwanza kupata Skendo mbaya Gazetini.
(5) Ana historia ya kuongea non stop toka mwanzo hadi mwisho wa safari, haijalishi umbali na pia ni Msanii ambaye anaiva na kila Msanii.
(6) Msanii pekee mwenye nyimbo nyingi zenye majina ya kike Duniani (kitabu cha Guinnes hakijamstukia tu)
OUTRO.
Dully ni mfano wa kuigwa mbele ya macho ya mbunifu yeyote sababu huwa haogopi kukosea na ambisheni zake ni zakuongoza sio za ukifuata upepo… hafati ispokuwa anafatwa, na pia ana ujasiri wa kuzitetea hisia na hata kuwaprove wrong wale waliokuwa wanapinga style yake ya Muziki na kuwanyamazisha wale wote waliokuwa wanampaka yeye ni Mwanasesere, Muuza sura tu au Mbana pua..
Wanamuita Mzazi wa Bongo Fleva kwasababu ni yeye ndie aliyeanzisha aina hii ya uimbaji ambao huwa una ladha ya kimwambao na zile za Bangra kwa mbaali (na kama una sikio zuri utagundua kuna vionjo vya kicongo vimeongezwa ili kutia Chachandu siku hizi) na amewainspaya WANABONGOFLAVA wengi na karibia wote wanalikubali hilo pasina kutaka mjadala au kuonyeshana uhodari wa maneno.
Dully anafurahia sana kuona WANABONGOFLAVA wapya wanavyofanikiwa kimaisha na pia anazikubali chalenji zao kwa moyo mweupe kabisa lakini anasema YEYE NI MKONGWE,KAMWE HATOKUBALI KUFUNZWA UTAMADUNI NA WATOTO.
Muziki kwake ni zaidi ya kipaji, yeye binafsi anaamini KIPAJI alichonacho ni kama ZAWADI aliyoshushiwa na Allah ili ajipatie rizki, anamaliza kwakusema ‘alijifunza yeye mwenyewe kupiga gitaa, keyboard na drumz,wala hakufundishwa na mtu yeyote’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment