Wednesday
MCHIZ AY APATA TUZO YA MSEKE
Kidume cha mzee Yesaya kinazidi kufanya poa katika huu ulimwengu wa muziki na kuisimamisha dede bendera ya Tanzania... Hapa namzungumzia kijana anayemiliki kampuni ya rubudani inayoitwa Unit Entertainment... Ni A.Y
Ameshinda tunzo ya East African song of the year kupitia wimbo wa LEO katika tunzo za Museke za Ghana.. Na leo hii anaenda Kampala kwa ajili ya kufanya show katika fainali za Pilsner Djs Spinning.
"Napenda kuwashukuru mafans wote walioni support kwa kunitakia kheri na kunipigia kura katika tunzo za Ghana zijulikanazo kwa jinala la Museke na kufanikiwa kushinda.. na ushindi huu si wa A.Y peke yake bali ni ushindi wa Tanzania, Mashabiki wa A.Y na mashabiki wa muziki kiujumla.. Nafanya kazi sana , mnanipa support kubwa na mafanikio bado hatujayafikia so mo faya" Hayo ni maneno ya A.Y
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
unatisha kaka ay mpk kieleweke ndo tukimbie.
Post a Comment