Saturday

AJALI ALIYOPATA BAHATI BUKUKU LEO ASUBUHI.

Muimbaji maarufu nchini wa nyimbo za injili nchini,Bahati Bukuku (40) amepata ajali akiwa katika gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kugonga gema, baada ya kugongwa na gari lingine linalosemekana kuwa ni fuso.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi watu wengine waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo mbali na Bahati Bukuku ni watu wawili na gari lililopata ajali na kusababisha majeraha
kwa watu hao ni Toyota Nadia yenye namba za usajili IT 7945.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema ajali hiyo imetokea july 25 saa tatu 9:00 alfajiri katika Barabara ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO wilayani Kongwa.
Uchunguzi wa ajali hiyo nado unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

Wednesday

Mh Lowassa akutana na balozi wa Ubelgiji

 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya mambo ya nje Mh Edward Lowassa akizungumza na balozi wa Ubelgiji Hapa nchini Koen Adam aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Saalam jana.Walijadiliana masuala mbalimbali yakiwemo suala la mchakato wa katiba mpya,mzozo katika eneo la nchi za maziwa makuu pamoja na hali katika Umoja wa Ulaya ilivyo kwa sasa.