Tuesday

SABABU ZA KIFO CHA KANUMBA ZATAJWA,BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUFANYIA UCHUNGUZU MWILI WAKE


MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.

PICHA MBALIMBALI ZA TASWIRA YA MSIBA WA KANUMBA

 hemed na mlela wakiingia msibani
 sehemu ulipokuwa mwlilin wa marehe kanumba
 baadhi ya wasanii wakiubeba mwili wa marehemu kanumba
 mwili ukiweka chini kwa maisha yake ya milele
 wakati mwili wake ukibebwa kuingia kabulini
mdada anayedaiwa kuwa chanzo cha kifo cha kanumba

WIZZ KHALIFA FREE STYLE


“JACKY DANIEL” NDIO ILIYOMUUA KANUMBA; UCHUNGUZI KUTOKA POLISI.

RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela Pombe kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi. ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba. Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia. Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu. “Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine. Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema Kamanda huyo. Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema. Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.

Thursday

LEO 1.Kila siku ni siku ya kujifunza jambo jipya iwe kwa kusikia,kuona au kupitia katika maisha. 2.Kuheshimu wengine. 3.Kuacha uoga,wengi wetu tuna uoga wa kufanya jambo fulani.Mfano kusimama na kuongea mbele za watu na mengine.Pambana na huo uoga pengine unakunyima nafasi ya kukua katika kujiamini. 4.Kujipenda mwenyewe kwanza. 5.Kuwapenda na kuwajali wengine wote wanaokuzunguka haijalishi upungufu walionao. 6.Kuwa mpenzi mwenye kukidhi mahitaji ya mpenzi wako.Ikiwemo kuwa mwaminifu,mkweli,kujali,kumheshimu mwenzako n.k 7.Kuwa mtu mwenye kusamehe. 8.Acha kulalamika juu ya matatizo yako,yafanyie kazi. 9.Tambua thamani yako. 10.Jishauri wewe mwenyewe,wakati mwingine huwa tunaomba ushauri kwa watu wengine huku tukiwa na majibu sahihi ndani ya mioyo yetu. Kwa leo ni haya tu japo yapo mengi.