Thursday


King wa filamu za kibabe pande za Hollywood, Marekani, Arnold Schwarzenegger, aliyewahi kukalia kiti cha gavana wa jimbo la California ameichakachua ndoa yake baada kuanguka dhambini na ‘bekitatu’ Midred Patricia Baena. Stori kutoka unyamwezini zinadai kuwa ndoa ya mbabe huyo wa filamu la ‘Terminator’ iliyodumu kwa miaka 25 ilifikia tamati wiki iliyopita kutokana na kitendo chake kinachodaiwa kuwa cha kipuuzi zaidi kwa kumla uroda na kumpa kibendi hausigeli wake huyo.

Licha ya jitihada kubwa aliyoifanya Schwarzenegger kwa kunywea na kumuomba msamaha mkewe Maria Shriver pamoja na familia yake yote lakini alijikuta akiangukia pua na hatimaye familia yake kusambaratika vipande vipande.

Mapema jana mbele ya wanahabari mkali huyo aliyeng’arisha nyota ulimwenguni kupitia filamu kambambe la 'Commando' alikiri kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa yao ni mtoto wa nje aliyezaa na bekitatu huyo miaka 10 iliyopita, jambo ambalo limeiacha dunia kwenye mshangao mkubwa.

Mildred Patricia Baena kwa miaka 20 alikuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwa mbabe huyo na alikuwa akipokea mshahara mzuri wa dola 1,200 sasa ana miaka 50 na ameshastaafu kazi na aliwahi kuwaambia marafiki zake kuwa alikuwa akifanya mapenzi na Arnold bila ya kutumia kinga Alipopata ujauzito hakumwambia Arnold ambaye baadae alikuja kugundua baada ya mtoto huyo wa kiume kuzaliwa na kufuatia kugundulika kwa siri hizo za ndani, mke wa Arnold,Maria Shriver mwenye umri wa miaka 55, ametangaza kuwa atatoboa siri zote atakapoenda kwenye shoo ya Oprah Winfrey baadae mwaka huu so usiikose endelea kufuatia hapa hapa G5 utaijua siku hiyo.

No comments: