Tuesday


FAIDA YA MAKALIO MAKUBWA

WANASAYANSI nchini Uingereza waliofanya utafiti wao katika Chuo Kikuu cha Oxford wamegundua kuwa makalio makubwa yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko matumbo makubwa.
Utafiti umeonyesha kuwa makalio na mapaja makubwa huhifadhi mafuta ambayo husaidia mwili kujilinda na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.
"Mafuta ya kwenye makalio na mapaja ni bora kwa afya lakini mafuta mengi ya kwenye tumbo si mazuri kiafya", alisema Dr Konstantinos Manolopoulos.
Dk huyo ni mmoja wa watafiti watatu walioshiriki kwenye utafiti huo ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la International Journal of Obesity.
Watafiti hao walisema mafuta ya kwenye tumbo hutoa tindikali nyingi za mafuta zenye madhara kwa mwili wakati mafuta ya kwenye makalio na mapaja huzuia tindikali za mafuta zenye madhara kuingia kwenye misuli na maini na hivyo kuuepusha mwili na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.
Ingawa mafuta ya kwenye makalio na mapaja huyeyuka taratibu sana lakini mafuta hayo hutoa homoni zenye faida zijulikanazo kama adiponectin ambazo huilinda mishipa ya damu na kusimamia kiwango cha sukari mwilini.
Wanasayansi hao walisema,wanaendelea na utafiti ili kutengeneza dawa za kuufanya mwili uhifadhi mafuta yake kwenye makalio na mapaja ili kupunguza matatizo ya kiafya yanayosababishwa mafuta kujazana kwenye tumbo.
Taarifa ya utafiti huo zimebainisha kwamba,wanawake wenye mapaja au makalio madogo sana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo kadhaa ya kiafya kama vile kisukari na magonjwa ya m