Tuesday


wanakijiji wetu wengi wanapenda sana

kulavizuri kuliko kufanya kazi,

mcheki kama huyu mama yeye

kaenda shamba kaacha kulima hiuyo

karudi na msosi bab'kubwa.

Monday


MSAIDIENI VICTOR, MAPENZI YANAMTATIZA
Pole na kazi dada yangu, naomba unipostie hii ili

mwenye experience hii anisaidie, mimi ni kijana
wa miaka 32 na ninafanya kazi kwenye benki moja
maarufu hapa Arusha(Stanbic), najua fika hili swali
ningelipeleka kwenye blog nyingine pengine ningepata
ushauri nasaha au wa kitaalam zaidi. Mimi nina swali kuhusu
wanawake wazuri kupita kiasi.
Kuna dada hapa town Arusha ni mzuri sana sana na kwakweli

nimevutiwa nae mno, anaelimu ya juu, na pia anafanya kazi
kwenye kampuni moja ya kimataifa, anaishi mwenyewe na
anajitegemea vizuri tu, ukimuona uzuri wake utasema ana
maringo sana lakini hapana, ni down to earth na ana upendo
wa hali ya juu wa kusaidia watu hata kama hawajui vizuri,
nimeshakutana nae mara kadhaa kama rafiki na nilisha
muaproach kimapenzi akanitolea nje, anasema hataki
kujihusisha sana kimapenzi sasa hivi ana taka kuconcentrate
na kazi yake kwanza, alikuwa na boyfriend wake wakaachana
mwaka jana, sasa nauliza ni wanawake wote wazuri wako hivyo?,
yaani wagumu kupata? yeye hana boyfriend kwasasa, kweli ni

mzuri sijawahi kuona, akiwa kwenye gari lake ndio ananimaliza
kabisa, sauti yake mh hata kama unamalaria unapona saa hiyo
hiyo, alienda ughaibuni mwaka jana kikazi nilikonda nikabaki
mifupa jinsi nilivyokua nammiss, sasa nakuuliza Dawson na wengine,
je hataki kuwa na mimi kwasababu anauwezo wa kujitunza au

uzuri wake ndio unamfanya awe anachagua sana, nimemzimia
nashindwa kulala, nashindwa kuconcentrate kwenye kazi zangu
kabisa, nimejitahidi kumsahau au kutokumuwaza nashindwa,
yaani najikuta bado namtaka yeye tu, msaada tafadhali.
Email yangu ni vshirima@gmail.com kwa anaetaka kunishauri zaidi.
Victor.





Papii na Baba yake Mzee Nguza wakirudishwa gerezani baada ya rufaa yao kushindikana. Picha mbili hapo juu kwa hisani ya (Khalfani Said wa TanzanPhotoBank. blogspot)

BARUA YENYEWE INASOMEKA KAMA IFUATATAVYO:

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.

Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu

Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki

Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

Na huo ndio mwisho wa barua alionitumia Papii ili imfikie Mh. Rais

Tahadhari:
Inaruhusiwa kuinakili hii story kama ilivyo ( i wont mind), ila sio vibaya pia mkitoa credit na sio kusema eti ni kutokana na vyanzo vyenu vya habari.
Walengwa mnajijua sio lazima nitaje majina

Isiwe kama mlivyofanya kwenye story ya TID kuchumbia na picha zangu za hospital mnanakili kila kitu na hamtoi hata shukrani.
Du! wizi wa story ni wizi pia jamani
Asante kwa blogs zingine kama u-turn na zinginezo wanaonesha shukrani na ushirikiano
Mimi pia huwa nashukuru kama nimepata kitu kwa mtu
Ni hayo tu

Saturday


Mimi ni mwanaume wa miaka 32, nimeoana na mke wangu sasa ni mwaka wa 4 na tuna mtoto mmoja. Nilikutana na huyu rafiki wa mke wangu miaka mitatu iliyopita tulipoamia Dar kikazi toka Mwanza nilipokuwa nafanyia kazi kabla. Nilipomwona tu nilimtamani na yeye hakuwa na hiyana, tukaanza mahusiano ya mapenzi kwa siri. Mahusiano yalipamba moto na siwezi kuhesabu ni mara ngapi nimefanya naye mapenzi. Kuna wakati nilitaka kuachana nae lakini alinitishia kuwa nikifanya hivyo ataharibu ndoa yangu, na ntakuwa nimekosa kila kitu. Nikiwa nae na mke wangu pamoja ninachoweza kufanya ni kutabasamu tu na siongei nae sana. Mke wangu anajuaga kuwa namchukia rafiki yake mana anaona huwa simchangamkii kivile kama wengine. Maskini, kumbe ni kinyume chake. Sasa nimechanganyikiwa mana ananiambia ana mimba yangu. Kwakweli sijui nifanyeje, mana nikifikiria tulipotoka na mke wangu na jinsi ninavyomsaliti kwa rafiki yake, roho inaniuma, ila ndo hivyo na naiweka ndoa yangu pabaya na nikifikiria na mtoto tena. Naomba wadau wa Mapenzi bongo wanipe ushauri.

Jamani naombeni msaada wenu nimeoa yapata mwaka wa 4 na tumejaliwa mtoto mmoja wa kike; Baada ya miaka miwili,Ndoa yetu imekumbwa na misukosuko mingi sana ikiwa ni pamoja na mwenzangu kupunguza kunipa haki yangu ya ndoa hadi kufikia miezi 3 (hapo kabla tulikuwa tukipumzika wakati akiwa kwenye period tu na mara nyingi sana yeye ndiye alikuwa akinichokoza; alianza na kunipunguzia ikawa mara moja kwa wiki; mara hataki tushiriki mchana ama asubuhi anataka usiku tuu na akiwahi kulalal hawezi kuamka tena na hata kwenda kuoga na mimi ndio kabisaaaa )na siku ya kupewa inakuwa kama anatimiza wajibu na ni round moja tu. Hali hii ilinishinda na kwa kweli niliamua kutoka nje ya ndoa yangu hii ikiwa ni baada ya kumsihi na kumtafadhalisha sana mke wangu juu ya jinsi nilivyokuwa najisikia nakereka ; jibu lake likawa yeye haoni tatizo na sio lazima tufanye mapenzi ndio nijue ananipenda!Hatimaye mke wangu akajua; sikumficha nilimweleza sababu na nikamwomba msamaha ikiwa ni pamoja na kumsihi kujali hisia zangu; hali ilitulia kidogo lakini masharti yakaongezeka aligoma nisimwendee chumvini na yeye akawa hataki kuniendea ilhali ni mchezo amabo mimi na yeye tumejifunza pamoja na tuliupenda sana hapo kabla; nilivumilia lakini miezi miwili baadae hali ikarudia kama ya zamani; nikitaka game nakuwa nafanya booking na mbaya zaidi style ikawa ni moja tu; kifo cha mende eti yeye ndo inamfurahisha zaidi lakini kibaya ikafikia nikitaka game lazima nimseme wee na siku nyingine nanyimwa tu bila hata maelezo; nikaamua kumfanyia upelelezi na kungamua kuwa alikuwa ana mahusiano yasiyo rasmi nje ya ndoa! nilikusanya ushahidi na kumface ambapo alikiri kufanya hivyo ikiwwa ni revenge kwangu eti haamini kuwa nimeachana na wanawake wa nje ; aliniomba msamaha nami kwa kukumbuka kuwa yeye ni mama mtoto wangu na alinisamehe huko nyuma ; nikamsamehe na tukaendelea kuishi; roho ilimiuma kwa kujutia niliyoyasabisha lakini niliamua kumsamehe ili kupona mimi binafsi. Tatizo limekuja sasa tumerudia hali hiyo tangu mwaka huu uanze nimepewa penzi mara moja; visingizio kila uchao mara kichwa kinauma mara tumbo limejaa gesi, mara period imekuwa ndefu mno hivyo napumzika ilimradi nashindwa kuelewa ikiwa bado ana mapenzi na mimi ama la ? Kwa kweli mimi nampenda sana na hasa has nikiona anavyomlea mwanetu na hata kunijali mimi kwa malazi na chakula; lakini namhitaji yeye kama mke wangu anchanganyikiwa nifanye nini!Kutoka nje tena sitaki kwani sikuona faida ya penzi la kuiba.Baba Rachel

Friday

Kumaliza hang-over
KICHWA kinagonga, unaona kizunguzungu, mwili hauna nguvu, unasikia kichefuchefu, kama unataka kutapika lakini hutapiki, kwa kifupi unajisikia hovyo kwa sababu ya unywaji wa kupindukia jana! Hali hii inaitwa HANG-OVER au uchovu.
Ingawa hatupendi kuelezwa ukweli au kufikiria madhara ya pombe, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa pombe ni dawa ya kulevya.
Ina dhoofisha mwili na pale mtu anapokunywa kupita kiwango, mwili hujawa na sumu.
Unapokutana na hali hiyo, mwili hujaribu kujinasua kama vile ambavyo kitu chochote kingefanya kinapovamiwa na kitu kigeni.
Njia bora ya kuondokana na uchovu (hangover) ni kunywa kiasi au kuacha kabisa ulevi.
Kama utashindwa kujizuia kunywa na unataka kujiepusha na uchovu asubuhi, ni vyema ukila vitu vifuatavyo ambavyo vinaweza kukusaidia:
1. NDIZI MBIVU
Unapozidiwa na kilevi, kiasi kikubwa cha madini ya potasiamu hupotea, hivyo kwa kula ndizi mbivu ambazo zinaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha madini hayo, kutakusaidia kupunguza makali ya hang-over.
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta ndizi mbivu nzuri, menya na kula kwa wingi.
2. TANGAWIZI
Tangawizi mbichi imekuwa ikitumika kwa muda mrefu kutibu magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya kusikia kichefuchefu na mafua.
Andaa juisi ya tangawizi mbichi na kunywa kama ilivyo, au unaweza kuandaa kwa kukata vipande kati ya 10 hadi 12 na uchanganye na vikombe 4 vya maji. Chemsha kwa dakika 10, epua na chuja.
Changanya na juisi ya chungwa moja, kipande cha limau na nusu kikombe cha asali.
Kunywa mchanganyiko huo utapata nafuu mara moja.
3. ASALI NA LIMAU
Asali na limau ni kinywaji bora kuliko vyote katika tiba hii, ni rahisi kutengeneza na kunywa.
Kinarudisha haraka kiasi cha sukari na maji kilichopotea wakati wa kunywa kilevi.
Chemsha maji kiasi cha kikombe kimoja, changanya limau na asali kupata ladha unayoitaka.
Ni bora kutumia asali ili kupata sukari ya asili, badala ya kutumia sukari ya kawaida.
Ili kupata ahueni, kunywa mchanganyiko huo mara kadhaa kwa siku.
4. SUPU, WALI
Mtu anapoanza kupata nafuu kutokana na uchovu, chakula huwa kitu cha mwisho kabisa kutamani kula, lakini pamoja na kutojisikia hamu ya kula, unahitaji kula ili mwili upate nguvu.
Unashauriwa kuanza kwa kula vyakula vyepesi kama vile wali mweupe, supu, n.k
5. KINYWAJI MAALUM
Kunywa pia vinywaji maalum vinavyotumiwa na wanamichezo kwa lengo la kurejesha nguvu na madini yaliyopotea mwilini.
Unaweza pia kunywa vinywaji vya kutia nguvu mwili (energy drink) kama vile, Red Bull, Shark, Malta Guiness, n.k
6. BARAFU
Ili kutuliza maumivu ya kichwa, chukua vipande vya barafu, weka kwenye mfuko wa plastiki ambao utazungurusha kwenye kitaulo na kuweka kwenye kipaji chako cha uso kinachogonga.
7. JUISI
Juisi, hasa fresh ya machungwa, husaidia kupandisha kiwango cha sukari kilichopotea na husaidia kuondoa dalili za uchovu mwilini.
Hata hivyo, kama tumbo lako limechafuka sana, kunywa juisi ya epo (tufaha) badala ya machungwa ambayo ina asidi.
8. MAJI
Mbali ya muda, maji ni tiba bora ya uchovu.
Upungufu wa maji unaotokana na kunywa kiasi kingi cha kilevi ndiyo unaoleta kasheshe mwilini. Kunywa maji mengi wakati wote wa mchana, siyo chini ya glasi nane kwa siku.
DONDOO MUHIMU
Ili kujiepusha na ‘hang-over’ asubuhi baada ya kunywa kupita kiasi, kunywa maji mengi sana kabla ya kupanda kitandani.
Au kunywa taratibu, kinywaji kimoja kila baada ya saa moja kwani huo ndiyo muda unaotumika na kinywaji kusambaa mwilini na kusambaa.
KWELI NYUMBA INA SIRI KUBWA SANA,USIONE MILANGO IMEFUNGWA LAITI UNGEJUA YANAYOENDELEA NDANI..KUTA TU NDIO ZINATUSITIRI.
Huyu mama amekuja ofisini leo mchana kiukweli amenisikitisha sana amelia sana.Kiukweli kumuona mtu mzima analalamika na kulia machozi juu ya matatizo yanayomkabili inasikitisha sana.Mama anasimulia matatizo yanayomkabili katika ndoa yake ya miaka 12.Ameishi miaka 12 na mumewe na wana mtoto mmoja kwa miaka 2 sasa haelewi kuhusu mumewe anasema amebadilika anamkaba usiku,anabadilika anakuwa anatisha kama mnyama anamkaba mpaka anakosa pumzi.Akimwambia mume wake kwa nini ana mfanyia hivyo anamuomba msamaha harudii tena lakini haachi ndio yamekuwa maisha yake kwa miaka 2 sasa.Anasema kila akijaribu kumuacha ndio mwanaume anazidiki kumfanyia vituko akienda kwao mwanaume anamfata hukohuko.Pia alikuwa akifanya hivyo kwa mtoto wao mpaka imebidi mama amuamishe mtoto asije akafa bure.Anasema akikusimulia utaona ni jambo la kawaida na utalichukulia juujuu lakini kiukweli anateseka sana na haelewi afanye nini.
mama hapo pichani akilia kwa uchungu kweli.
Sasa anamekuja anaomba ushauri hajui afanyaje anatamani hata kufa.Mimi kiukweli niliogopa mpaka nikasema hili suala tukiliongea kwenye Romanticsky mumewe akisikia si atakudhuru kama mambo yenyewe ndio hayo akasema hajali bora jamii isikie imshauri afanye nini.Tunamsaidiaje kimawazo pia kesho sikiliza kwenye mitaa yetu............
Kuna siku nilikuwa nimepita mahali nikawa nimekaa namsubiri mtu,sasa pembeni yangu kulikuwa na meza ambayo wamekaa wanaume 7.Baada ya muda akaja jamaa ameongozana na mwanamke akawa amefika katika ile meza akawa anawaambia wale majamaa 7 kuwa ametoka leo ameamua kuja pale na wife...majamaa wakamkaribisha shemeji yao na kuhakikisha anapatiwa huduma zote.Sasa kilichoendelea ni kwamba yule dada akawa hayupo sehemu ya mazungumzo pale.Wale wanaume wakaanza kuongea mambo yao ya mpira,siasa na mengine ya kikazi.Dada wa watu akawa anachezea tu simu yake na kucheka kidogo na kuongea mara chache pale anapoweza kuongea lakini kwa kumtazama alikuwa bored.
Sasa leo kwenye leo tena nikahoji hali kama hii inapokutokea umetoka na mpenzi wako lakini huko anakutana na marafiki zake 3 au 4 mnakaa na kujumuika nao wewe unakuwa katika hali gani?unaenjoy?
MSG zilizoingia baadhi:
1.Kwa mimi sitajisikia vizuri maana nitaboreka na maongezi

Thursday


mtoto mzuri Zamalad wa Clods Fm

diva kwenye usiku wa merod and romance

rihanna nae haishi vituko

Naomi Campblle akiwa na pozi tata

tyrese

hii tena nayo toka kulekule Hait

kama moyo wako mdogo usiangalie

TID alipopata mchumba akamtngaza mbele ya wadau

ray C n Lady jay D

tamasha la Zinduka
hey check lijisong hili

0

NISHIKE MKONO LYRICS....."KWA TANDY"...KILA KHERI, MUIMBIE UMPENDAE WEEK END HII

Chorus:
Nishike mkono, kwani mimi ndie wako
Mpenzi tafadhali, usiniache mbali x2

Sahau kuhusu mwili, nimeshakupa moyo
Na nimekukubali we ua langu la roho
Twende kote uendako, moyo wangu uko kwako
Wao waseme wasemayo, nimekuridhia wa moyo

Siangalii pembeni, nisije kukwaza we mpenzi
Sitaki penzi la pili, we ndie wangu wa kweli

Chorus:

Yapata miaka saba, lakini ni kama forever
Mola amenishushia, naomba usije badilika
Nitakuwa na wewe milele, tuangalie ya mbele
Tusije haribu penzi wakasema, kumbe hatuwezi

Kama nilivyo ahidi, katu sitovunja ahadi
Nakukabidhi tena, moyo wangu ushauteka

Nishike mkono kwani mimi ndie wako
Mpenzi tafadhali, usiniache mbali

Wimbo umeimbwa na Lady JayDee na Mad Ice
Umeandikwa na Judith Wambura Mbibo

Thursday