Papii na Baba yake Mzee Nguza wakirudishwa gerezani baada ya rufaa yao kushindikana. Picha mbili hapo juu kwa hisani ya (Khalfani Said wa TanzanPhotoBank. blogspot)
BARUA YENYEWE INASOMEKA KAMA IFUATATAVYO:
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki
Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
Na huo ndio mwisho wa barua alionitumia Papii ili imfikie Mh. Rais
Tahadhari:
Inaruhusiwa kuinakili hii story kama ilivyo ( i wont mind), ila sio vibaya pia mkitoa credit na sio kusema eti ni kutokana na vyanzo vyenu vya habari.
Walengwa mnajijua sio lazima nitaje majina
Isiwe kama mlivyofanya kwenye story ya TID kuchumbia na picha zangu za hospital mnanakili kila kitu na hamtoi hata shukrani.
Du! wizi wa story ni wizi pia jamani
Asante kwa blogs zingine kama u-turn na zinginezo wanaonesha shukrani na ushirikiano
Mimi pia huwa nashukuru kama nimepata kitu kwa mtu
Ni hayo tu

No comments:
Post a Comment