Pages

Monday


MSAIDIENI VICTOR, MAPENZI YANAMTATIZA
Pole na kazi dada yangu, naomba unipostie hii ili

mwenye experience hii anisaidie, mimi ni kijana
wa miaka 32 na ninafanya kazi kwenye benki moja
maarufu hapa Arusha(Stanbic), najua fika hili swali
ningelipeleka kwenye blog nyingine pengine ningepata
ushauri nasaha au wa kitaalam zaidi. Mimi nina swali kuhusu
wanawake wazuri kupita kiasi.
Kuna dada hapa town Arusha ni mzuri sana sana na kwakweli

nimevutiwa nae mno, anaelimu ya juu, na pia anafanya kazi
kwenye kampuni moja ya kimataifa, anaishi mwenyewe na
anajitegemea vizuri tu, ukimuona uzuri wake utasema ana
maringo sana lakini hapana, ni down to earth na ana upendo
wa hali ya juu wa kusaidia watu hata kama hawajui vizuri,
nimeshakutana nae mara kadhaa kama rafiki na nilisha
muaproach kimapenzi akanitolea nje, anasema hataki
kujihusisha sana kimapenzi sasa hivi ana taka kuconcentrate
na kazi yake kwanza, alikuwa na boyfriend wake wakaachana
mwaka jana, sasa nauliza ni wanawake wote wazuri wako hivyo?,
yaani wagumu kupata? yeye hana boyfriend kwasasa, kweli ni

mzuri sijawahi kuona, akiwa kwenye gari lake ndio ananimaliza
kabisa, sauti yake mh hata kama unamalaria unapona saa hiyo
hiyo, alienda ughaibuni mwaka jana kikazi nilikonda nikabaki
mifupa jinsi nilivyokua nammiss, sasa nakuuliza Dawson na wengine,
je hataki kuwa na mimi kwasababu anauwezo wa kujitunza au

uzuri wake ndio unamfanya awe anachagua sana, nimemzimia
nashindwa kulala, nashindwa kuconcentrate kwenye kazi zangu
kabisa, nimejitahidi kumsahau au kutokumuwaza nashindwa,
yaani najikuta bado namtaka yeye tu, msaada tafadhali.
Email yangu ni vshirima@gmail.com kwa anaetaka kunishauri zaidi.
Victor.




No comments:

Post a Comment