KWELI NYUMBA INA SIRI KUBWA SANA,USIONE MILANGO IMEFUNGWA LAITI UNGEJUA YANAYOENDELEA NDANI..KUTA TU NDIO ZINATUSITIRI.
Huyu mama amekuja ofisini leo mchana kiukweli amenisikitisha sana amelia sana.Kiukweli kumuona mtu mzima analalamika na kulia machozi juu ya matatizo yanayomkabili inasikitisha sana.Mama anasimulia matatizo yanayomkabili katika ndoa yake ya miaka 12.Ameishi miaka 12 na mumewe na wana mtoto mmoja kwa miaka 2 sasa haelewi kuhusu mumewe anasema amebadilika anamkaba usiku,anabadilika anakuwa anatisha kama mnyama anamkaba mpaka anakosa pumzi.Akimwambia mume wake kwa nini ana mfanyia hivyo anamuomba msamaha harudii tena lakini haachi ndio yamekuwa maisha yake kwa miaka 2 sasa.Anasema kila akijaribu kumuacha ndio mwanaume anazidiki kumfanyia vituko akienda kwao mwanaume anamfata hukohuko.Pia alikuwa akifanya hivyo kwa mtoto wao mpaka imebidi mama amuamishe mtoto asije akafa bure.Anasema akikusimulia utaona ni jambo la kawaida na utalichukulia juujuu lakini kiukweli anateseka sana na haelewi afanye nini.
mama hapo pichani akilia kwa uchungu kweli.
Sasa anamekuja anaomba ushauri hajui afanyaje anatamani hata kufa.Mimi kiukweli niliogopa mpaka nikasema hili suala tukiliongea kwenye Romanticsky mumewe akisikia si atakudhuru kama mambo yenyewe ndio hayo akasema hajali bora jamii isikie imshauri afanye nini.Tunamsaidiaje kimawazo pia kesho sikiliza kwenye mitaa yetu............
No comments:
Post a Comment