0
NISHIKE MKONO LYRICS....."KWA TANDY"...KILA KHERI, MUIMBIE UMPENDAE WEEK END HII
Chorus:
Nishike mkono, kwani mimi ndie wako
Mpenzi tafadhali, usiniache mbali x2
Sahau kuhusu mwili, nimeshakupa moyo
Na nimekukubali we ua langu la roho
Twende kote uendako, moyo wangu uko kwako
Wao waseme wasemayo, nimekuridhia wa moyo
Siangalii pembeni, nisije kukwaza we mpenzi
Sitaki penzi la pili, we ndie wangu wa kweli
Chorus:
Yapata miaka saba, lakini ni kama forever
Mola amenishushia, naomba usije badilika
Nitakuwa na wewe milele, tuangalie ya mbele
Tusije haribu penzi wakasema, kumbe hatuwezi
Kama nilivyo ahidi, katu sitovunja ahadi
Nakukabidhi tena, moyo wangu ushauteka
Nishike mkono kwani mimi ndie wako
Mpenzi tafadhali, usiniache mbali
Wimbo umeimbwa na Lady JayDee na Mad Ice
Umeandikwa na Judith Wambura Mbibo
No comments:
Post a Comment